Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde amemtaka Spika Job Ndugai ajiuzulu kufuatia kauli aliyoitoa kupinga serikali kuchukua mikopo. Lusinde amesema alianagalia clip yote ya mazungumzo ya Job Ndugai na hakuna sehemu iliyounganishwa ili kumchonganisha na Rais kama yeye (Ndugai) alivyosema, alieleza zaidi kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake na hivyo hata katika uombaji wake wa msamaha hakuwa na sababu ya kukanusha alichokisema. Lusinde amemtaka Spika Ndugai kujiuzulu mara moja ili kuwatendea haki wagogo pamoja na wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao ni wanufaika mkubwa wa mkopo uliochukuliwa na serikali.