Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Lupembe atoa pikipiki 12 za thamani ya Mil 30 kwa Makatibu Kata CCM.
MAKATIBU Kata kumi na mbili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamefanikiwa kupatiwa pikipiki mpya kila mmoja ambazo zitawasaidia kufanya kazi za chama hicho kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 na uchanguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa madiwa,wabunge na rais.
Ametoa pikipiki kumi na mbili zenye thamani ya Milioni 30, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe leo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda ambapo amesema kuwa ametoa pikipiki hizo kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake.
Mbunge Lupembe amesema kuwa pikipiki hizo zitawasaidia Makatibu Kata wa CCM kwenye ujenzi wa chama hicho hasa kuongeza wananchama wapya.
Amesema kuwa hapo awali tayari ameshatekeleza ahadi nyingine ya kutowa Milioni moja kwa kila ofisi ya CCM Kata Jimbo la Nsimbo ambapo yote kwa pamoja amelenga kuimashari chama kiutendaji ili kufikia ushindi kwenye uchaguzi ujao.
Aidha ametoa ahadi nyingine ya kuhakikisha kila kiongozi wa ngazi ya chini atapatiwa baiskeli kwa ajili ya kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Katavi,Iddy Kimata licha ya kumsifu mbunge huyo kwa kutowa pikipiki amesema makatibu kata wanapaswa kutambua kuwa pikipiki hizo ni mali ya CCM na hawataruhusiwa kuzitumia tofauti na kazi walizopangiwa.
Kimata amesema kuwa anatambua kazi kubwa inayofanywa na mbunge Lupembe hivyo kazi kubwa inayofanywa ni kwa sababu ya mshikamo waliona Wanakatavi.
“Hizi ni pikipiki mpya ni mali ya Chama Cha Mapinduzi na kadi zake zitandikwa kwa jina la CCM na sio pikipiki za katibu,mwenyekiti au mwenezi yeye binafsi kwahiyo rai yangu kwenu pokeeni pikipiki hizi na mzifanyie kazi iliyokusudiwa kama mbunge anavyotaka iwe” Amesema Kimata.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo amefafanua “Tunaenda kwenye uchaguzi maana yake ni kwamba makatibu kata wetu,wenyeviti na waenezi wafike kila mahali kwenye maeneo yao ya kata”.
Aidha ameeleza kuwa mahala ambapo pikipiki hizo zitatumika vibaya Chama kichukue pikipiki hiyo na ihifadhiwe katika ofisi ya CCM Wilaya kwani hatarajii kuona pikipiki zikiwa bodaboda na Katibu wa Chama Wilaya anatakiwa kuwasimamia.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki amempongeza Mbunge Lupembe kwa jitihada zake za kukijenga chama huku amemuunga mkono kwa kutoa kiasi cha fedha Jumla ya Tsh 350,000/= kwa Makatibu kata CCM ili waweze kuweka mafuta.
Martha amesema kuwa pikipiki hizo zitatumika kwa makusudi yaliyopangwa ili kuendelea kukijenga chama hasa kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa na uchanguzi mkuu.
Akizungumza kwa niamba ya Makatibu Kata CCM,Mrisho Yunus amemshukuru Mbunge Anna Lupembe kwa kutimiza ahadi yake ambapo amesema wanatambua sababu ya kupewa pikipiki hizo kwamba ni kwa ajili ya ujenzi wa Chama.
Hivyo amesema watafanya kazi kwa ufanisi zaidi za kisiasa ili kukipatia ushindi chama kwenye changuzi zijazo.