Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MAHAWANGA AZINDUA KIWANDA CHA USHONAJI KATA YA WAZO
Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Janeth Elias Mahawanga ameungana na mamia ya Wanawake wa Tawi la Kisanga Kata ya Wazo kuzindua mpango wa uanzishwaji Kiwanda cha ushonaji kama mradi wa Tawi hilo katika kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na uzinduzi huo pia lilifanyika tukio kubwa la kuwapokea Wanachama wapya wa UWT ambao wengi wao wanafurahishwa na kazi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi sambamba na fursa mbalimbali zinazowalenga Wanawake katika masuala mazima ya kuwainua kiuchumi.
Mhe. Janeth Elias Mahawanga amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayofanya pamoja na kurudisha fursa ya mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu na kuwataka wanufaika hao kuchangamkia fursa hii sambamba na kubuni miradi yenye tija ambayo itapelekea pesa hii kutopotea badala yake kutengeneza ajira na kuinua vipato vya Watanzania.
Mh. Janeth Elias Mahawanga amewataka Wanawake wote kutoka Matawi 14 yanayounda Kata ya Wazo kuhakikisha kila Tawi linakuwa na mradi ili waweze kujitengenezea ajira miongoni mwao na kuondokana na utegemezi. Vilevile amewaomba Viongozi kuwa wabunifu hata kama niwa ngazi ya Tawi kwani wananafasi kubwa ya kuionyesha jamii kile walichonacho pamoja na kuwa wanaongoza ngazi ya Matawi.
Mh. Janeth Elias Mahawanga aliendelea kusisitiza na kutoa rai yake kwa Wanawake kuhakikisha wanaungana katika kutafuta maendeleo ya pamoja na kuwahakikishia
kuwakutanisha kwenye vikao vyao na wadau muhimu wa maendeleo kama Sido, TBS, Kampuni za Bima, Taasisi za Kifedha, Brella, TIC, Maafisa Biashara wa Halmashauri na Wataalam wa Masoko ili kuwapa uelewa mpana wakati wakiendelea na taratibu za kukamilisha mradi huo.
Mwisho, Mh. Janeth Elias Mahawanga aliwasisitiza Wanawake wenzake kuendeleza upendo na mshikamano katika safari ya kuelekea kwenye chaguzi zijazo lakini pia kugombea nafasi mbalimbali bila woga. Vilevile amewahakikishia Wanawake wa Tawi la Kisanga kuwa nao bega kwa bega mpaka mradi wao utakapokamilika kwani kiu yangu kubwa ni kuona maendeleo makubwa ya Wanawake ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.06.jpeg40.7 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.06(1).jpeg52 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.06(2).jpeg45.2 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.07.jpeg50.2 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.07(1).jpeg38.5 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.07(2).jpeg56 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2023-08-14 at 11.25.07(3).jpeg44.8 KB · Views: 3