Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MARTHA GWAU AHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA WILAYA YA MKALAMA, SINGIDA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Marha Nehemia Gwau amefanya ziara Wilaya ya Mkalama na kupokelewa kwa shangwe na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake wa Wilaya ya Mkalama
Mhe. Martha Nehemia Gwau ametembelea jengo la nyumba ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) linaloendelea na ujenzi hatua ya lenta na kuahidi kutoa vifaa vya kufunga lenta na kumalizia ujenzi ili hatua ya kuezekeka bati iendelee.
Aidha, Mhe. Martha Nehemia Gwau amegawa vitendea kazi vya Ofisi kwa Makatibu wa Kata ili wakafanye kazi katika mazingira rahisi kwa kuwapa Kalamu, Mafaili, Rimu na Notebook
Pia, Mhe. Martha Nehemia Gwau ametembelea Shina Namba 7 la Kitongoji cha Barabarani Kijiji cha Miganga na kupandisha bendera na baada ya hapo amefanya mkutano wa hadhara Kijiji cha Miganga kwaajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Vilevile, Mhe. Martha Nehemia Gwau alisikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi ambapo ameendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutumia Nishati Safi ya kupikia bila kuathiri Misitu na kugawa Majiko ya Gesi kwa Mama Lishe.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.18.00(1).jpeg374.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.20.44.jpeg408.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.20.43.jpeg470.1 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.23.10.jpeg411.1 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.23.11(2).jpeg421.5 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.23.12.jpeg462.4 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.27.10(2).jpeg414.1 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.27.11(2).jpeg446.7 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.32.38.jpeg557.4 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.35.14(1).jpeg589.7 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.37.15(2).jpeg365.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 09.37.18(1).jpeg397.8 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 12.42.30.jpeg231.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-30 at 12.42.27(1).jpeg178.4 KB · Views: 3