Mbunge Martha Gwau Awagusa Wanawake wa Singida DC & Ikungi kwa Majiko ya Nishati ya Gesi ya Kupikia

Mbunge Martha Gwau Awagusa Wanawake wa Singida DC & Ikungi kwa Majiko ya Nishati ya Gesi ya Kupikia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE MARTHA GWAU AWAGUSA WANAWAKE WA SINGIDA DC & IKUNGI KWA MAJIKO YA NISHATI SAFI YA GESI YA KUPIKIA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Nehemia Gwau amekabidhi majiko ya Gesi 60 kwa wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Wilaya ya Ikungi Disemba 21,2024 Ikiwa ni mwendelezo wake wa kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa wananchi.

Akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mbunge Gwau amewagusa wanawake kwa kuwapa Majiko ya Gesi Kata ya Ilongero, Kijota na Mtinko akisema kuwa ameleta Majiko hayo ili kuwasaidia wanawake watumie nishati safi ya kupikia kama ambavyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyohimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Rais Samia amelipa kipaumbele sana matumizi ya gesi mbadala ya kupikia, anatamani kila mmoja awezekutumia nishati hii ndio maana na sisi wasaidizi wake tunaendelea kumuunga mkono ndio maana leo natoa mitungi ya gesi" Mbunge Martha Gwau

Vilevile, Mbunge Martha Gwau ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu akitaka amani hiyo iendelee katika maisha yao yote kama ambayo waasisi wa taifa hili walivyo acha amani na utulivu.

"Nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kufanya uchaguzi kwa amani pamoja na hayo basi tuilinde amani yetu iliyopo hapa nchini kama tulivyoachiwa urithi na waasisi wa taifa hili" Mbunge Martha Gwau

Aidha, Mbunge Martha Gwau amewashukuru viongozi mbalimbali ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ndani ya jimbo kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwa kushirikiana vyema na madiwani wote wakiwemo wa viti maalumu.

Pia, Mbunge Gwau baada ya Ilongero akatoa mitungi ya Gesi kijiji cha Kideka kilichopo Kata ya Puma Wilaya ya Ikungi kwa wafanyabiashara pamoja na kofia kwa ajili ya kujikinga na jua pamoja na pochi za kuwekea pesa zao.

Mbunge Martha Gwau amepongeza juhudi za Serikali na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.
 

Attachments

  • Screenshot 2024-12-24 at 12-23-53 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-23-53 Instagram.png
    838.6 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-24-08 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-24-08 Instagram.png
    844.7 KB · Views: 2
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-24-31 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-24-31 Instagram.png
    876.4 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-23-38 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-23-38 Instagram.png
    898.3 KB · Views: 2
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-23-21 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-23-21 Instagram.png
    818 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-23-08 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-23-08 Instagram.png
    892.9 KB · Views: 2
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-22-54 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-22-54 Instagram.png
    955.2 KB · Views: 2
  • Screenshot 2024-12-24 at 12-22-42 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-24 at 12-22-42 Instagram.png
    866.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom