Ukizungumzia uchapaji kazi, unamaanisha nini??
Uchapakaji kazi unaozungumziwa ni hule wa kuwa na uwezo wa kuweza kulitumikia Taifa lako na kuleta maendeleo kwa wanchi wako kwa namna moja au nyingine.
Sasa isije kuwa nawe unajiweka katika wale wanaochapa kazi ukiwa na matumaini ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa kuteuliwa
Haya nipe sifa Tano bora ambazo Mkuu aliwateua wafuatao
Makamba ni mbunge wa kuteuliwa na hapo hapo bado ni katibu wa chama cha Mafisadi, lakini ni wazi kuwa mzee huyu haya uwezo kabisa wa kufanya kazi walau moja kiufasaha kabisa, zaidi ya porojo tu, na hilo CCM mnalitambua (nukuu Kikwete akiongea na wazee Diamond pale juzi) sasa ukimpa kazi mbili zinajoitaji kushirikisha ubongo atafanya kweli?? Naomba vigezo na sifa za ufanisi za Makamba
Haya Mchungaji G. Rwakatale, huyu naye unaweza kutoa sifa zake zilizomchukulia Mh. kumteua kuwa mbunge, kama sio kucheza na madaraka waliompa wananchi, toa siafa za huyu mama!!
Haya Meghi, ndio bure kabisa, na aliteuliwa na Kikwete na akapewa na uwaziri, lakini kama utakumbuka alidhubutu kusema kuwa alidanganywa na Balali kusaini Vijisenti vya BOT, wakati yeye alipewa katiba na mwongozo wa serikali na kuhudhulia ngurudoto, sasa utasemaje kuwa Kikwete anajua sifa za hawa jamaa ndio maana anawateua??
wako wengine wengi tu ambao nao no vilaza, ila nalazimika kusema kuwa, inawezekana hata President nae ndio wale wale ndio maana hata watu anaowachagua ni wa aina hiyo, kwahiyio msishangae, kwani hajafanya lolote likafanikiwa toka achukue upresident, zaidi ya kuonyesha usanii, na big failure kila siku ni kuchagua mijitu bure kabisa na pumba kichwani