Mbunge Masache awataka waumini kutii mamlaka

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Mhe. Masache Kasaka amewasihi waumini wa dini ya kikristo kusoma maandiko ya kibiblia na kuyatendea kazi ikiwemo agizo la kutii wenye mamlaka na kuwaombea kama viongozi wa dini na Serikali.


Mbunge Masache amepata nafasi ya kutoa nasaha hiyo aliposhiriki ibada katika kanisa Katoliki Kigango cha Chalangwa, ambapo amenukuu andiko kutoka kitabu cha Tito. 3:1 kinachosema "Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema"


Pia, Mhe. Masache amechangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa unaondelea, huku akisisitiza wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya Serikali za mitaa.

 
Imeandikwa,

Itiini mamlaka Kwa kuwa IPO kutisha waovu,

Sasa mamlaka kama IPO kutisha wenye HAKI na kushirikiana na wezi, hiyo mamlaka corrupt ni ya kuifukuza kabisa.

Yaani tuitii mamlaka inayotia kura fake kwenye Sanduku la kura?

Msitumie BIBLIA vibaya🙏
 
Yesu mwenyewe wanayemuamini hakutuu mamlaka ya Warumi hadi wakamuua akasome maandiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…