Mbunge Mavunde aja na mkakati Kabambe kuwawezesha Wanadodoma kiuchumi

Mbunge Mavunde aja na mkakati Kabambe kuwawezesha Wanadodoma kiuchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
-Kufadhili uanzishwaji wa kiwanda kimoja kidogo kila mwaka

-Kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi

-Wanawake,Vijana na wenye ulemavu kupewa Kipaumbele

-Amshukuru Rais Samia kurejesha mikopo ya asilimia 10

Mbunge wa Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde, amebainisha kuwa Jimbo lake la Dodoma Mjini litakua linatenga Sh Milioni 20 kila mwaka kwaajili ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi kwa ajili ya manunuzi ya mashine na mitambo midogo kwa lengo kuzalisha bidhaa na kuongeza thamani kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Mei 2024 na Mhe Anthony Mavunde (Mb) wakati wa akizindua wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoratibiwa na Jeshi la Polisi pamoja na Kanisa Halisi la Mungu Baba, Jijini Dodoma.

“Kutokana na nia ya dhati ya Rais wetu mpendwa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua Wananchi kiuchumi amerejesha tena ile mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba na hii itawasaidia kuondokana na mikopo kausha damu.

Ili mkopo huo ulete tija,ni lazima tuwaandae wana Dodoma kupata mafunzo ya ujasiriamali na ujuzi mbalimbali wa uzalishaji bidhaa kupitia mafunzo kama haya ya leo.

Kwangu kama Mbunge nimekuja na progamu ya kukiinua kikundi kimoja kila mwaka kwa kutoa Tsh 20,000,000 ya ununuzi wa mashine na mitambo kuanzisha viwanda vidogo vidogo”Alisema Mavunde

Kiongozi Mkuu wa Kanisa halisi la Mungu Baba Askofu Baba Halisi Ameishukuru Serikali na viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana nao kwa karibu na kueleza dhumuni la mafunzo haya ni kuiandaa jamii kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Taifa.

Hapo awali akimwakilisha Afande RPC Mkoa wa Dodoma Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Afande Eva Michael Stesheni, ameipongeza Kanisa la Mungu Halisi kwa kuja na wazo hilo la kuwainua Wananchi kiuchumi kwani linaenda sambamba na mipango iliyopo katika Jiji la Dodoma na kwamba kupitia mafunzo haya idadi kunwa ya wanajamii itapata ujuzi wa kushiriki katika uzalishaji mali na hivyo kupunguza vitendo vya uhalifu katika jamii.

WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.44.56.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.44.56(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.44.59.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.44.59(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.44.59(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.45.00.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.45.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.45.00(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.45.01.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-21 at 19.45.02.jpeg
 
-Kufadhili uanzishwaji wa kiwanda kimoja kidogo kila mwaka
Sasa Tsh 20 Million ndiyo za kuanzisha kiwanda? Huyu naye sijui wanampaga uwaziri kwa vile kabila lake ni Mgogo? Maana ni empty set kabisa.

Hiyo ni mtaji wa saloon za akina mama mitaa ya Buza au Mburahati
 
MBUNGE MAVUNDE AJA NA MKAKATI KABAMBE KUWAWEZESHA WANADODOMA KIUCHUMI

- Kufadhili uanzishwaji wa kiwanda kimoja kidogo kila mwaka.

- Kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi.

- Wanawake, Vijana na wenye ulemavu kupewa Kipaumbele.

- Amshukuru Rais Samia kurejesha mikopo ya asilimia 10.

Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, amebainisha kuwa Jimbo lake la Dodoma Mjini litakua linatenga Sh Milioni 20 kila mwaka kwaajili ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi kwa ajili ya manunuzi ya mashine na mitambo midogo kwa lengo kuzalisha bidhaa na kuongeza thamani kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Hayo yamebainishwa tarehe 22 Mei, 2024 na Mhe. Anthony Mavunde (Mb) wakati wa akizindua wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoratibiwa na Jeshi la Polisi pamoja na Kanisa Halisi la Mungu Baba, Jijini Dodoma.

“Kutokana na nia ya dhati ya Rais wetu mpendwa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua Wananchi kiuchumi amerejesha tena ile mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba na hii itawasaidia kuondokana na mikopo kausha damu.

Ili mkopo huo ulete tija,ni lazima tuwaandae wana Dodoma kupata mafunzo ya ujasiriamali na ujuzi mbalimbali wa uzalishaji bidhaa kupitia mafunzo kama haya ya leo.

Kwangu kama Mbunge nimekuja na progamu ya kukiinua kikundi kimoja kila mwaka kwa kutoa Tsh 20,000,000 ya ununuzi wa mashine na mitambo kuanzisha viwanda vidogo vidogo” Alisema Mavunde

Kiongozi Mkuu wa Kanisa halisi la Mungu Baba Askofu Baba Halisi Ameishukuru Serikali na viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana nao kwa karibu na kueleza dhumuni la mafunzo haya ni kuiandaa jamii kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Taifa.

Hapo awali akimwakilisha Afande RPC Mkoa wa Dodoma Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Afande Eva Michael Stesheni, ameipongeza Kanisa la Mungu Halisi kwa kuja na wazo hilo la kuwainua Wananchi kiuchumi kwani linaenda sambamba na mipango iliyopo katika Jiji la Dodoma na kwamba kupitia mafunzo haya idadi kunwa ya wanajamii itapata ujuzi wa kushiriki katika uzalishaji mali na hivyo kupunguza vitendo vya uhalifu katika jamii.
 
Attachments

  • IMG-20240521-WA0043.jpg
    IMG-20240521-WA0043.jpg
    63.5 KB · Views: 4
  • IMG-20240521-WA0047.jpg
    IMG-20240521-WA0047.jpg
    100.5 KB · Views: 4
  • IMG-20240521-WA0046.jpg
    IMG-20240521-WA0046.jpg
    148.3 KB · Views: 4
  • IMG-20240521-WA0045.jpg
    IMG-20240521-WA0045.jpg
    71.8 KB · Views: 3
  • IMG-20240521-WA0044.jpg
    IMG-20240521-WA0044.jpg
    116.4 KB · Views: 4
  • IMG-20240521-WA0052.jpg
    IMG-20240521-WA0052.jpg
    63.8 KB · Views: 3
  • IMG-20240521-WA0051.jpg
    IMG-20240521-WA0051.jpg
    132.3 KB · Views: 6
  • IMG-20240521-WA0050.jpg
    IMG-20240521-WA0050.jpg
    47.6 KB · Views: 5
  • IMG-20240521-WA0049.jpg
    IMG-20240521-WA0049.jpg
    110 KB · Views: 4
  • IMG-20240521-WA0048.jpg
    IMG-20240521-WA0048.jpg
    94.9 KB · Views: 3
Uchaguzi umekaribia ndio anakurupuka alikua wapi miaka yote mitatu nyuma 🤔 kuongoza waswahili ni rahisi sana 😁
 
Kipindi cha kuelekea uchaguzi mambo mengi hutokea - J Makamba
 
Back
Top Bottom