Mbunge mavunde awapa tabasamu watu wenye ulemavu

Mbunge mavunde awapa tabasamu watu wenye ulemavu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
▪️Agawa viti mwendo 20 kwa wanafunzi na wenye ulemavu

▪️Mbunge Keisha apongeza juhudi za Mbunge Mavunde kwa watu wenye ulemavu

𝐃𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amegawa vitu mwendo 20 kwa wanafunzi na wananchi wenye ulemavu Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu Jijini Dodoma.

“Imekuwa ni utamaduni wangu kila mwaka kusaidia makundi yenye mahitaji maalum juu ya upatikanaji wa vifaa saidizi ikiwemo viti mwendo.

Leo nipo hapa kukabidhi viti 20 ambavyo wadau wa maendeleo wametuunga mkono kwa ajili ya wanaDodoma na hasa wanafunzi ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu kutokana na ukosefu wa viti mwendo”Alisema Mavunde

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu(SHIVYAWATA)Dodoma Ndg. Hassan Lubuva amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwa karibu na watu wenye ulemavu wa Dodoma na kutoa rai kwa mashirika na watu binafsi kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.

Akizungumza katika makabidhiano hayo,Mbunge Mwakilishi wa Watu wenye ulemavu Mh. Khadija Shaaban Taya amemshukuru Mh Mavunde kwa kuwa kimbilio la watu wenye ulemavu na kutoa wito kwa wadau wengine kusaidia upatikanaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu.

WhatsApp Image 2024-10-31 at 09.27.23.jpeg
WhatsApp Image 2024-10-31 at 09.27.25.jpeg
 
Back
Top Bottom