KERO Mbunge Mavunde, tusaidie wakazi wa mtaa wa Chinyoyo, kata ya Kilimani - Dodoma! Tunateseka sana barabara mbovu sana

KERO Mbunge Mavunde, tusaidie wakazi wa mtaa wa Chinyoyo, kata ya Kilimani - Dodoma! Tunateseka sana barabara mbovu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tafadhali ndugu Mavunde tusaidie sisi wakazi wa mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani tunateseka sana na ubovu wa barabara.

Kata ya kilimani ina mitaa mitatu, Uzunguni, Chinyoyo na Image! Cha kushangaza mtaa wa uzunguni(kwa vibopa) kumwtandazwa lami tupu hadi taa za barabarani zimewekwa!

Mtaa wa Image, barabara za lami zipo tele na hata zile za vumbi zinakarabatiwa karibu kila mwaka. Ila kwa sisi wakazi wa Chinyoyo barabara ni mbovu sana na tunapata tabu sana hususani kipindi cha mvua.

Kwanini kunakuwa na double standard kwa kata moja? Mitaa mingine wana barabara nzuri sana, wakati wakasi wengine hata kupita mnapita kwa tabu sana! Madimbwi ndio madimbwi!

Barabara ni kama vile hakuna kabisa! Tusaidieni ndugu Mavunde na sisi tujione tunathamimiwa kama wenzetu wa uzunguni (ama sababu wao ni mtaa wa vigogo?)

Lakini na sisi tunalipa kodi vile vile!
 
Mavunde yupo Dar huko Anapokea wageni wa Nishati, pambaneni na hali zenu.
 
Yuko tayari achangie pesa, yule domo wa yanga abakie bongo, nyie wengine mtajijua
 
Mlimpenda wenyeww, chaguo lenu wenye,
Wacha muisome namba eeh, kwa ujinga wenu, mavunde mbele kwa mbele 😂
 
Back
Top Bottom