Maswa Yetu
Senior Member
- Mar 18, 2023
- 155
- 217
Jimbo la Chato ni kama limetelekezwa na mbunge wake Medard Kalemani kwani toka atumbuliwe kwenye nafasi yake ya waziri wa nishati amegeuka bubu.
Chato ilijengwa stendi nzuri sana ya mabasi lakini leo ni mwaka wa nne toka ikamilike lakini haitumiki! Yani wananchi wa Chato wanateseka kwa kuchomwa na jua kwenye stendi ya mavumbi wakati stendi nzuri yenye kila kitu ipo. Kinachosikitisha zaidi ni mbunge Medard Kalemani kukalia kimya jambo hili.