Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ABUBAKAR ASENGA AMEIOMBA SERIKALI KUONDOA MGOGORO WA ARDHI KILOMBERO
Mbunge wa Jimbo la Kilombero (CCM), Mhe. Abubakar Asenga ameiomba Serikali ikamsaidie kupima ardhi ya wananchi ili akwepe laana ya Askofu.
Mhe. Abubakar Asenga ametoa kauli hiyo Alhamisi Mei 25,2023 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mhe. Abubakar Asenga amesema katika Jimbo lake kuna mgogoro wa siku nyingi kati ya wananchi na Kanisa Katoliki ambao unahitaji busara ya Serikali baada ya Askofu kuamua kuacha mgogoro.