Nitashangaa sana kama wajumbe na wanasheria maili wakiacha na hili lipite tu. Ninavyojua ili uwe mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unahitaji kuchaguliwa ama kuteuliwa na baadha ya kutangazwa mshindi unaenda mchakato wa mwisho ambapo unaapishwa na Spika wa bunge mbele ya kikao cha Bunge. Sasa binafsi natambua Mheshimiwa Mgimwa Junior ni Mbunge Mteule wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Jimbo la Kalenga mara baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi. Lakini nijuavyo kwa sasa bunge maalum la katiba linaendelea na hivyo hakuna vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo vitamfanya Mhe. Mgimwa kuapishwa. Sasa Je Spika ataitisha kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano ili kumwapisha? Pili Je atakuwa na nguvu ipi kuingia Bunge la katiba huku akiwa Bado hajatimiza matakwa ya kisheria ya kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano?
Najua kama inalazimu ale kiapo Spika na Serikali hawashindwi kuitisha Bunge la Jamhuri ya Muungano hata kwa Dk tano na wakapata posho na kumwapisha na kisha kurihairisha ili mradi kumfanya atimize sifa za kisheria kuingia bunge maalum la katiba. Je ingekuwa kwa mfano kachukua mbunge wa Upinzani, Bunge linaweza kufanya chochote kwa dharura katika hali kama hii?