Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Maji ni Uhai hatimaye Wananchi wa kitongoji cha Songoloji wapata huduma ya Maji baada ya maagizo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo alipofanya ziara yake tarehe Februari 28, 2023 na wananchi wa Shina namba 13 walimwelezea kero ya ukosefu wa huduma ya maji ambapo aliibeba kero hiyo na kuifanyia kazi, hapo hapo aliweza kuchangia Milioni 1,200,000 kwa ajili ya kununulia vifaa vya kujenga miundombinu. Pia aliagiza viongozi kuhakikisha zoezi hilo la ujenzi wa DP linakamilika mapema sana.
March 02, 2023 hii viongozi wa Chama na Serikali kutoka Wilaya ya Ikungi wakiongozwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Thomas Apson Mwang’onda wameweza kutimiza agizo hilo na sasa wananchi wanapata huduma ya maji.