Tatizo si mbunge peke yake, ni system nzima iliyombeba. Kuanzia DC, RC, RPC, OCD, Msimamizi wa jimbo nk. Hao mapolisi wengine walikuwa wanatekeleza amri tu. Na kwakweli system ni mbovu kabisa na imelelewa hivyo tangu 1995.
Mwl Nyerere ndiye alisababisha yote haya pale aliposhindwa kuona ni vipi CUF itawale Zanzibar na CCM itawale serikali ya muungano. Tunakumbuka aliposhinikiza CCM itangazwe mshindi zanzibar. Tangia hapo CCM wakajua kuwa unaweza ukashindwa bado ukajitangaza mshindi na kwa kuwa unazo nguvu za dola basi hakuna atakayekusumbua - ni ubabe huhuo wanaouendeleza hadi sasa. Hakika iko siku historia itamhukumu Nyerere. Naomba vatican wachunguze kwa makini kabla ya kumtaja kuwa mtakatifu!