Mbunge Mwambe: Ujio wa Rais Mtwara utatatua Migogoro

Mbunge Mwambe: Ujio wa Rais Mtwara utatatua Migogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Ndanda Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Mhe. Cecil Mwambe, amewataka wananchi wa Chikunja na Likuredi wajitokeze kwa wingi kumlaki Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakapokuwa anaelekea Nachingwea mkoani Lindi.

Mwambe ameyazungumza Septemba 14, 2023 wakati wa mapokezi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa anawasili mkoani Mtwara kwenye ziara yake ya siku 4.

"Niwaombe sana wananchi wa Likuredi na Chikunji mjitokeze kwa wingi kumpungia mkono Rais lakini ikimpendeza anaweza akasimama maeneo hayo na kiwasalimia na mimi kama mbunge wao nitakuwepo kwasababu bado tuna kero kwenye maeneo hayo naamini tukipata nafasi basi tutamueleza"

Aidha, Mwambe amekiri kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu kwa wananchi wa vijiji vya Nangalole kata ya Namajani na Magereza licha ya kuzungumziwa hadi bungeni hivyo anaamini ujio wa Rais Samia utatatua changamoto hiyo.

IMG-20230914-WA0102.jpg
 
Samia hataki hiyo,ya eti yeye akija,ndo mimwambie matatizo,yeye atawaambia,kuna viongozi mnao,wafikishieni hayo matatizo.
 
Back
Top Bottom