Mbunge Mwita Getere acharuka: Ukiwa Mbunge unakuwa na akili, ukipata tu Uwaziri unajisahau. Rais ameteua mfanyakazi gani?

Mbunge Mwita Getere acharuka: Ukiwa Mbunge unakuwa na akili, ukipata tu Uwaziri unajisahau. Rais ameteua mfanyakazi gani?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini (CCM) Boniphace Mwita Getere amewataka baadhi ya Mawaziri kutimiza wajibu wao kwa weledi ili kuweza kutatua changamoto za wananchi.

Getere ameyasema hayo Ijumaa Februari 7, 2025 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2024 na taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2024.

"Rais amewateua mfanye kazi gani, amewateua mtusaidie sisi wabunge, wakati fulani huwa ninajiuliza maswali mengi sana, mtu akiwa mbunge wa kawaida anakuwa na akili nyingi sana akiwa Waziri anajisahaulishasahaulisha, kwanini mnakuwa hivyo?" Amesema.

 
Back
Top Bottom