Mbunge na Mwanamuziki, MwanaFA apinga sheria mpya ya BASATA ya kutaka kusikiliza nyimbo kabla ya Msanii kuipeleka redioni. Asema ni ya ‘kidwanzi’

Mbona kuna nyimbo nyingi kwa mfano za Wcb zimejaa matusi na huwezi kusikiliza hata na Mzazi ama mtoto wako na hawajazifungia
Umeambiwa hii sheria utekelezaji wake umeenza tar 1 May 2021
 
Haya mambo yapo Tanzania tu mamaqe. Hivi aliyeturoga nani? Kabisaaaa eti ukitoa wimbo peleka BASATA!! Hahahahah mbona tumerudi kwenye Ujima na Ujamaa.
Kiongozi,ukiacha Pm,( ambayo haipatikani) njia gani nyingine naweza kukufikia.ahsante
 
MKIACHA MATUSI KWENYE MZIKI WENU Mtapungukiwa nini?

BaSATA nanyie hamtaki mistari ya kuwakosoa na serikali... Kwani nyie Mungu?
 
Mkuu tafadhali,umeielewa vyema hiyo post?
Mkuu tafadhali,umeielewa vyema hiyo post?
Mkuu nimeilewa sana, kwa muda mrefu serikali imekuwa ikitumia njia rafiki kuwashauri hawa wasanii wazingatie maadili kwenye kazi zao lakini wameshindwa. Sasa serikali imeamua iongeze mbinyo wa kisheria ambapo tangu may mosi mwaka huu utekelezaji wa sheria hii umeanza. Huyu msanii amekuwa akiimba nyimbo za matusi "refer wimbo wake wa mwanaume suruali" alioimba na Vanessa mdee. Analalamika kitu gani zaidi ya kulilia kuimba matusi.
 
Kwanini asiyaongelee bungeni?
Me nahisi wakati mwngine mbinu ya kusolve tatizo ni kuliwahi likiwa la moto. Kuongea bungeni ni rotation wako wabunge wengi so mpaka aje aongee ni unakuta muda umesogea. Kuanza kuandika mtandaoni nahisi ni hatua ya kwanza. pia naona kaongea hasahasa kutokana na msukumo uliotokana na nyimbo ya ney. Me naona kafanya vizuri na asiishie hapa aende akaliongelee bungeni.
 
Huu ni mwanya wa rushwa kwa watumishi wa BASATA, utoe hongo ndio nyimbo ipewe go ahead
Na hii iko hivyo hivyo katika taasisi na ofisi nyingi za serikali, hawana namna ya kujiendesha wamejazana ofisi cha maana wanachofanya hakuna na wanataka wajiendeshe kwa nguvu za wananchi kwa kulazimisha urasimu. Kuna taasisi nyingi sana za serikali zinazofanya kazi inayofanana, au taasisi kubwa ila inafanya kazi "ndogo" ambayo ingeweza kupelekwa kwenye taasisi nyingine iwe idara.
 
Wangesema tu mtu apeleke shairi lake au tungo yake kabla ya kuanza kurecord na asahihishwe kama inabidi harafu akabithiwe kwenda kurecord

Lkn hii amesharecord ndo alete hahahaha wataua vipaji sana

Lkn pia wanapaswa kusimamia maadili ya kitanzania kwa nguvu zote
 
Sheria ni ya kijinga, inatengeneza mazingira ya rushwa hapo BASATA, inaua ubunifu, inaua sanaa.

Tulishatoa namna nzuri ya wao kuchuja maudhui ila wamekaza mafuvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…