Mbunge Nancy Nyalusi alia na Madeni ya Wakandarasi yanayopelekea riba kubwa kwa Serikali

Mbunge Nancy Nyalusi alia na Madeni ya Wakandarasi yanayopelekea riba kubwa kwa Serikali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
ampongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na kikosi kizima cha Wizara ya Ujenzi. Sote tumeona jinsi ambavyo Mvua zimeharibu miundombinu kwa mwaka huu lakini wamehangaika usiku na mchana kuhakikisha huduma zinarejea kwa wananchi, tunawapongeza sana na kuwatia moyo, tuna imani na matarajio makubwa na ninyi" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Mkoa wa Iringa tumepokea miradi mingi ya maendeleo katika Wizara ya Ujenzi. Barabara ya Ipogolo - Kilolo (KM 63), Serikalini zilitolewa Shilingi Bilioni 63 kwaajili ya ujenzi na Mkandarasi tayari yupo kazini na ujenzi unaendelea kwa kasi kubwa" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Barabara ya Mlima Kitonga kutokana na maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, Mlima Kitonga Barabara ilikuwa haipitiki, magari ya mizigo yalikuwa ni mengi na kulikuwa na msongamano mkubwa. Tulikuwa tunashuka kwa Nusu Saa lakini tulikuwa tunatumia zaidi ya masaa manne hadi masaa matano kushuka na kupanda kwenye Mlima Kitonga. Tunaishukuru Serikali kwa kutoa Shilingi Bilioni 6.5 kwaajili ya kufanya marekebisho kwenye kona kali za Mlima Kitonga na upembuzi yakinifu unaendelea ili tuweze kupata Barabara bora zaidi" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Tunaishukuru Serikali imetupatia Barabara ya Iringa - Pawaga (KM 20) na sasa tupo kwneye mchakato wa kumtafuta Mkandarasi ili ujenzi uanze katika Barabara hiyo" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Mkoa wa Iringa tuna changamoto, Barabara ya Ihemi kuelekea Usokami, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi tunaomba utusaidie maana Barabara haipitiki, ina mashimo, wananchi wanalalamika. Hata ukitufanyia marekebisho ya kawaida ili wananchi waweze kupita na kupata huduma zao za kila siku" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Mheshimiwa Rais alipokuja Mkoa wa Iringa alitupa ahadi ya kutujengea Barabara ya lami KM 10 kutoka Kinanyambo A hadi Madibila. Waziri utuambie umefikia wapi katika kufanyia kazi ahadi ya Mheshimiwa Rais ili wananchi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini waweze kupata matumaini" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Mwaka 2022 tulisaini mkataba wa Barabara ya Mafinga - Mgololo na Mkandarasi alikabidhiwa eneo. Wote tulifurahi kuwa tunakwenda kupata Barabara lakini ni mwaka mmoja hamna kitu chochote kinachoendelea, Barabara ni mbaya, haipitiki, wananchi wanateseka. Barabara ya Mufindi ndiyo tunaitegemea kwa shughuli za kiuchumi. Ni lini utamlipa Mkandarasi Advance Payment ili aendelee na kazi" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Kuna changamoto katika Wizara ya Ujenzi ambayo ni madeni ya Wakandarasi yanayopelekea riba kubwa kwa Serikali yanayoongezeka mwaka hadi mwaka na wanalipwa madeni haya ni Wakandarasi wa nje. Mwaka wa fedha 2021/2022 tumelipa riba ya Shilingi Bilioni 36.8; Mwaka 2022/2023 tumelipa riba ya Bilioni 44. Waziri tuambie, hiki ni kitu cha kawaida au ni sawa?

WhatsApp Image 2024-05-30 at 12.39.06.jpeg
 
Back
Top Bottom