Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NANCY NYALUSI ASISITIZA WAZAZI KUONGEZA UMAKINI WA MALEZI YA WATOTO WAO
"Tunalala nao, tunakula nao, tunaenda nao shambani; sasa hivi kuna baadhi ya watu roho ya utu hawana tena. Mtu anaweza akamuingilia mtoto wa mdogo wake, mtoto wa dada yake. Hali ni mbaya, nawaomba Mama zangu tuzingatie uslaama wa watoto wetu" - Mhe. Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Naowaomba sana Mama zangu tuzingatie na tunzungumze na watoto wetu kwa upole ili wawe huru kutuelezea kitu kinachoendelea kwenye maisha yao"
"Nawapongeza akina Mama wa Kata ya Makungu kwa namna mnavyopambana kujiinua kiuchumi, nimesikia mna vikundi vya ujasiriamali, mnajichangisha fedha, mnakopeshana ili kila mtu ajiinue kwa kile anachofanya, hongereni sana"
"Nawachangia kikundi cha Kirumaruma cha Wajasiriamali Shilingi 200,000 ili muongeze mtaji katika shughuli zenu za kiuchumi. Hongereni sana Mama zangu"
Aidha Mhe. Nancy Hassan Nyalusi alisisitiza juu ya Wananchi wote kushiriki Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na Daftari la Mkazi ambalo ni lazima Kujiandikisha kwenye vitongoji, vijiji na kwenye maeneo yote.
Vilevile, Mhe. Nancy Nyalusi alisema kuwa ili tuweze kumpa kura za kutosha Mheshimiwa Rais, Mbunge, Diwani na Wenyviti wa Vijiji ni lazima Kujiandikisha na kuwaomba Daftari litakapofika watatangaziwa na viongozi hivyo wajitokeze kwa wingi.