Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Ndaisaba Ruhoro achangiwa fedha za kuchukua fomu ya ubunge na wanawake zaidi ya 400 wa kabanga.Wanawake zaidi ya 400 wa Mji mdogo wa Kabanga waliandaa Hafla ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. NDAISABA G RUHORO kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuiwakilisha Ngara.
Hafla hiyo iliyofanyikia Kabanga kwenye ukumbi wa Free Park Hotel iliambatana na ukataji na ulaji wa Keki ambapo walaji walitoa TZS 500 kwaajili ya kumchangia Mhe. Ruhoro kuchukua fomu ya kugombea UBUNGE wa Jimbo la Ngara Mwaka 2025.
Mbali na kundi hili yapo makundi mengine ambayo yamepanga kumchangia fedha za kuchukua fomu ya UBUNGE Mhe. Ndaisaba George Ruhoro kwenye uchaguzi mkuu ifikapo mwaka 2025.
Soma Pia:
- Mbunge Ndaisaba Ruhoro achangia Tsh. Milioni 8 kwa UVCCM Wilaya ya Ngara
- Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka
RUHORO amewashukuru sana wananchi wote wa Jimbo la NGARA kwa Imani na mapenzi makubwa sana waliyonayo juu yake na anaendelea kuwaahidi kuwatumikia kwa viwango vya juu na kwa unyenyekevu mkubwa.
Wenu; Ernest RUHUGU
Katibu wa Mbunge
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-09-02 at 20.21.42.jpeg326.3 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-09-02 at 20.21.45.jpeg355.2 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-02 at 20.21.47.jpeg193 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-09-02 at 20.21.51.jpeg311.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-02 at 20.21.53.jpeg181.2 KB · Views: 6