Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliver Daniel Semuguruka, wamehitimisha kampeni za wagombea nafasi za uongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji katika Kata ya Nyamiaga, Wilaya ya Ngara.
Katika hotuba yake, Mhe. Ndaisaba Ruhoro aliwahimiza wananchi kufahamu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo, akibainisha kuwa maendeleo ya jamii yanategemea uongozi bora unaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Amehimiza kuchagua viongozi makini wa CCM ambao watakuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo ya Nyamiaga.
Aidha, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro alisisitiza umuhimu wa kutunza kura, akiwataka wananchi kuhakikisha kura zao zote zinakwenda kwa wagombea wa CCM. "Tusikubali kuharibu hata kura moja, tunataka kijani na njano tupu," alisema, akisisitiza mshikamano na uzalendo kwa chama hicho.
Wananchi wa Nyamiaga wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuhakikisha viongozi bora wanapatikana kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kata hiyo.
PIA SOMA
- LIVE - LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024