Mbunge Ndaisaba Ruhoro achangia Tsh. Milioni 8 kwa UVCCM Wilaya ya Ngara

Mbunge Ndaisaba Ruhoro achangia Tsh. Milioni 8 kwa UVCCM Wilaya ya Ngara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara Mkoa wa Kagera ameshiriki Baraza la Kikanuni la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) la Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera.

Mhe. Ndaisaba George Ruhoro Ametoa Shilingi Milioni 5 (5,000,000) kwaajili ya Kununua Simu za Usajili wa Kielektroniki kwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata 22 na Milioni Tatu (3,000,000) mchango wa Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi.

Vilevile, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amezindua Tawi la Wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ngara Mjini ambapo amesisitiza vijana kuendelea kukijenga Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake (Wazazi, UVCCM na UWT).

WhatsApp Image 2024-09-02 at 11.48.02.jpeg
 
Hongera kwa mbunge. ndio kati ya wabunge walioko karibu na wanachi
 
Back
Top Bottom