Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE RUHORO AKABIDHI VYETI VYA MAFUNZO YA UDEREVA KWA VIONGOZI WA CCM ZAIDI YA 150
Ngara; 2/12/2024
Kufuatia kukamirika kwa mafunzo ya Udereva yaliyo tolewa na Chuo cha Lake Zone Driving College kwa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Ngazi za Kata Wilayani Ngara Chini ya Uratibu wa CCM mkoa na Wilaya, Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh NDAISABA RUHORO ameshiriki hafra ya kuwatunuku vyeti wahitimu zaidi ya 150.
Mh NDAISABA RUHORO alidhamini mafunzo hayo kwa kutoa TZS 4,350,000.00 ambayo ilitumika kama ada ya mafunzo kwa kila mushiriki ambaye ni kiongozi wa CCM. Baada ya kutunukiwa vyeti, sasa wahitimu hao wanaanza kusaidiwa kutafutiwa leseni za Udereva ambapo Jimbo la Ngara ni jimbo la pili ambalo linatoa huduma za Leseni za Udereva ndani ya Mkoa wa Kagera. Hivyo wahitimu watapata huduma za leseni hapa hapa Ngara.
Wakati wa hafla hiyo, Mh RUHORO aliwaeleza wahitimu kuwa, Mafunzo hayo yalitolewa kutokana na uongozi mzuri wa DR Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ameboresha utendaji kazi wa Viongozi wa CCM jambo ambalo limefanya viongozi hao kupata mafunzo ya udereva pamoja na stadi nyingine za Maisha.
Mh RUHORO amewaomba wahitimu hao kuwa Askari wa Miguu wa Mstari wa Mbele (Frontline Foot Soldiers) katika kusaka ushindi wa CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao hasa hasa ushindi wa DR SAMIA Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nao wahitimu wametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Ngara Mh NDAISABA RUHORO pamoja na Katibu wa CCM wa Wilaya ya NGARA Bi Anastazia Amas Amosi kwa utendaji kazi mzuri na namna wanavhojitolea katika kuhudumia wananchi na Wanachama wa CCM Ngara.
Wenu
Ernest RUHUGU
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Ngara