Mbunge Ndaisaba Ruhoro Alilia Serikali Bei ya Mahindi

Mbunge Ndaisaba Ruhoro Alilia Serikali Bei ya Mahindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo kunusuru zao la Mahindi ambalo bei yake inashuka siku hadi siku.

Mhe. Ndaisaba ametoa kauli hiyo baada ya wananchi kuibua kero hiyo kwenye mkutano wa hadhara alioufanya Kata ya Ngara mjini ambapo wameeleza kuwa wanatumia gharama kubwa kulima lakini bei ya mahidi kwa kilo ni shilingi 250 hadi 180 kwasasa.

Wananchi wamesema kuwa wamekuwa wakinunua mbegu kilo 2 kwa shilingi elfu 2 na gharama nyingine za uendeshaji huku wakiishia kupunjwa Bei ya sokoni.

Kufuatia kilio hicho Ndaisaba amemuomba Waziri wa kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuwatuma NFRA Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula kufika wilayani Ngara ili kuweza kununua Mahindi hayo.

Kero nyingine iliyoibuliwa ni kuhusu umeme ambapo wnanachi wameomba kupewa huduma hiyo kwa Bei nafuu kutokana na maisha yao kuwa ya chini.

1719241648444.png

PIA SOMA
- Mbunge Ndaisaba Ruhoro: Mfanyabiashara wa Soko la Sukari Anauza Kilo Moja kwa Tsh.10,000. Hatuwezi Kukubali Wananchi Wetu Kuteseka

- Mbunge Ndaisaba Ruhoro Aililia Serikali Sakata la Kikokotoo
 
Wabunge hawana maana kuwepo Kwenye katiba yetu....ni wanasiasa wapiga kelele wasio na tija Kwa mwananchi
 
Mkuu ni kwel wananunua mbegu kilo 2 kwa elf 2 au ni typing error tu,
Serikal inabid ifanye namna maan mahind saiz hayana bei kabisa wakulima lazima walie
 
Back
Top Bottom