Mbunge Ndaisaba Ruhoro Asema Wakulima wa Kahawa Wataendelea Kunufaika

Mbunge Ndaisaba Ruhoro Asema Wakulima wa Kahawa Wataendelea Kunufaika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE WA JIMBO LA NGARA MH. NDAISABA RUHORO AKONGA MIOYO YA WAKULMA WA KAHAWA

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro amehudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Ushirika Ngara Farmers Cooperative Society 2024-2025.

Akizungumza na Wakulima pamoja na Wanachama wa Ngara Farmers wapatao 960, Mheshimiwa Ndaisaba ameeleza mafanikio Katika zao hilo kwa kipindi cha Miaka 4 tangu kupewa ridhaa ya Ubunge 2020.

Amesema Katika msimu wa 2021 hadi 2024 jumla ya kilo milioni 7, laki 8 therathini na 6 elfu,na themanini na 5 (7,836,085) zenye thamani ya shilingi Bilioni 29,milioni 471,laki 5 na elfu 76 (29,471,576,000) zilizalishwa.

Akizungumzia jitihada za kuongeza tija Katika zao hilo la kibiashara amesema ikiwa Wananchi wa Ngara watampa Ushirikiano, atahakikisha kuwa Katika kipindi cha Ubunge wake kuanzia 2025-2030 Wakulima wa Kahawa wananufaika zaidi.

Ametoka makisio ya kipindi kijacho 2025-2030 kuwa Uzalishaji wa Kahawa utakuwa kilo milioni 13, Laki 7 na elfu 13, na mia 149 (13,713,149) zenye thamani ya shilingi Bilioni 109,milioni 709, laki 1 na elfu 90 (109,705,190,000).

Katika hatua nyingine za kuboresha Kilimo cha Kahawa, Mheshimiwa Ndaisaba amesema kufikia Mwaka 2030 atahakikisha Wakulima wamegawiwa Miche ya Kahawa kama ifuatavyo:-

1. Msimu wa 2020-2026, Miche 1,878,000 na,

2. Msimu wa 2026-2030 Miche 3,550,000 ikiwa ni Ongezeko la 10% kila Mwaka.

#NGARA TV UPDATES
#KAHAWA NI UTAJIRI 💰 💰 💰 💰 💰 💰
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-02-06 at 16.20.29.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-06 at 16.20.29.jpeg
    86 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-02-06 at 16.20.43.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-06 at 16.20.43.jpeg
    42.9 KB · Views: 2
Kule Kilimanjaro na Arusha walisha Ng'oa mikahawa ya Arabic yebye ubora kuliko hoo Rubusta, vipi hao wakukima wa Ngara wananufaika vipi?
 
Back
Top Bottom