Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Kutokana na kikao cha Wazee wa wastaafu na Mh Ruhoro kilichofanyika hivi karibuni nyumbani kwake Buhororo ambapo watumishi wastaafu walimtuma mbunge wao kuwapigania, Leo Mbunge wa Jimbo la Ngara ameiomba serikali kuboresha kiwango cha Pensheni ya wastaafu.
Ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kufanya kima cha chini cha Mushahara kuwa kima cha Chini cha Pensheni inayolipwa kila mwezi. Hii ni kwa sababu kuna wastaafu wanalipwa pensheni kiduchu chini ya laki moja na nusu hivyo kushindwa kumudu Gharama za Maisha.
Mh Ruhoro anaendelea kubeba agenda za watumishi wote wa Ngara wakiwemo wanaoendelea na kazi na wale waliokwisha sitafu serikalini kuhakikisha wanapata fedha ma malipo yanayokidhi mahitaji ya kila siku kwa watumishi.
Vile vile ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kufanya mapitio ya hitaji la ongezeko la pensheni kila mwaka baadala ya utaratibu wa Sasa wa kila baada ya Miaka mitatu hali ambayo inawaumiza wastaafu kwa kusubilia zaidi ya miaka mitatu ya serikali kufanya mapitio wakati wakiendelea kuapata malipo kidogo.
Mbunge RUHORO amekuwa kinara wa kuwapigania watumishi wilayani ngara na matunda yanaonekana hasa kwenye ongezeko la Madaraja, Kuikataa Bodi ya Kitaaluma ya Walimu, kuunda Umoja wa Wazee wastaafu Ngara, kuwagawia mitungi ya Gesi kila shule na mengine mengi
Soma Pia: Mbunge Ndaisaba Ruhoro Aililia Serikali Sakata la Kikokotoo
Mimi nasema ASANTE RUHORO kwa kuwapigania wazee wetu waliotumikia Taifa kwa ustadi mkubwa.
Wazee na watumishi wote wameshuhudia utumishi wako kwao na namna unavyojitoa kwa ajili yao.
Wenu
Ernest Ruhugu
Katibu wa Mbunge