Mbunge Ndaisaba Ruhoro Awasilisha Hoja za Maafisa Ugani Bungeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE NDAISABA RUHORO AWASILISHA HOJA ZA MAAFISA UGANI BUNGENI​

Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro leo tarehe 09 Mei, 2025 bungeni jijini Dodoma amefikisha mahitaji ya maafisa ugani ili waendelee kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Katika maswali yake, Ndaisaba Ruhoro ameiuliza Serikali juu ya uwezeshaji wa mafuta na mahitaji mengine kwa maafisa ugani lakini pia na kuiomba Serikali kuandaa mfuko maalum ili kuwawezesha maafisa ugani nchini wakiwemo wa Jimbo la Ngara.

Aidha, Ndaisaba George Ruhoro ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani imefanya maboresho mbalimbali ili kuinua wananchi hasa wakulima na kuiomba Serikali kuendelea kuboresha mahitaji ya Maafisa ugani nao waweze kuwafikia wananchi hasa Wakulima mashambani na kutoa Elimu ya kilimo chenye tija.
 
Huu ni uhuni yaani maafisa ugani wajaziwe mafuta ili waende kuzurura? Hii ni ajabu sana
 
Reactions: Lax
unafatilia maafisa ugani mpaka unanyoosha mikono - - - mamlaka ziliangalie hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…