Mbunge Ndaisaba Ruhoro: Watanzania puuzeni migomo kwa kuwa haina mashiko

Mbunge Ndaisaba Ruhoro: Watanzania puuzeni migomo kwa kuwa haina mashiko

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301


Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. NDAISABA G RUHORO amewaomba watanzania kupuuza watu wachache wanaohamashisha maandamano nchini hasa wale wanaotumia mitandao kufanya vikao vya kichochezi

Mbunge Ruhoro aliyasema haya alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara, Kijiji cha Kumubuga, Kata ya Nyamagoma, Wilaya ya Ngara tarehe 29.9.2024

Mhe. RUHORO amesema kuwa sababu za kufanya watu waandamane hazipo na hivyo mipango ya watu wanaohamasisha maandamano haitafanikiwa.

Mhe. Ndaisaba George Ruhoro Amesema kuwa watanzania wana UHURU wa kutumia Ardhi kuzalisha vyakura tofauti na baadhi ya nchi ambapo Ardhi inamilikiwa na watu wachache na kufanya watu wengi kuteseka tofauti na Hali ilivyo Tanzania.

"Kutokana na Sera Nzuri za CCM na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya DKT Samia Suluhu Hassan watanzania wanazalisha vyakura Vya kutosha na kusaza hadi kuwauzia majirani zetu. Kwa namna hii watanzania hatuna sababu ya kuunga mkono watu wanaotaka kuleta vurugu ili kuwafanya watanzania walale njaa"

Mbunge Ruhoro amesema watanzania wana UHURU wa kutumia Mito, Maziwa na Bahari kwenye uvuvi jambo linalowafanya kujipatia mboga na kipato Bila kusumbuliwa na mtu yeyote. Yapo Mataifa yenye Sheria ngumu na maeneo mengi Mito na maziwa yanasimamiwa na wawekezaji na hivyo kuwanyima fursa wananchi wa Kawaida tofauti na ilivyo hapa Tanzania.

Mbunge Ndaisaba George Ruhoro Amesema kuna nchi hasa zile zenye machafuko na migogoro ya mda mrefu UHURU wa kutembea umeminywa. Amesema kwa sasa Mtanzania akitaka kwenda kutembea hana kizuizi chochote kile ni yeye na nauli yake.

Ndaisaba George Ruhoro Amesema hata kwenye kufuga mifugo, Watanzania tuna UHURU wa kutosha kwenye kufuga mifugo. Watu wanafuga kuku, Bata, Kondo, Mbuzi na Ng’ombe kwa UHURU wa kutosha kabisa. Kuna mataifa hairuhusiwi kufuga Bila kupewa kibali na idadi ya mifugo hasa Ng’ombe wasizidi watano tafauti na Hali ilivyo Tanzania.

Mwisho; Ndaisaba George Ruhoro Amesema kundi Dogo lenye Tamaa na uchu wa Madaraka linalosema eti ‘’SAMIA MUST GO’’ lipo ndotoni tena ndoto za Abunwasi na halitafanikiwa kamwe kwa kuwa Samia Yupo na Atakuwepo Madarakani kwa mjibu wa Katiba.
 
Back
Top Bottom