Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NGARA: MICHE YA KAHAWA YAGAWIWA KWA WANANCHI WILAYANI - NGARA
Mhe. Ndasaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara amefika kwenye vitalu vya Kahawa na kushuhudia ugawaji wa Miche hiyo katika Vitalu vinavyopatikana katika Jimbo la Ngara ikiwa ni pamoja na kitalu cha Kata ya Nyakisasa kilichopo kijiji cha Kashinga.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameambatana na Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngara na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya, Wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Maafisa kutoka Ofisi ya Ugani na Kilimo
Ndugu Vitaris Ndailagije, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ngara amewasisitiza wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani ndicho Chama chenye uwezo wa kuleta maendeleo na kinaendelea kuleta maendeleo kwa watu
Naye, Bi Anasitazia Amas, Katibu wa CCM Wilaya ya Ngara ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Wananchi kwenda Kujiandikisha kwenye Daktari la Mkaazi kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amesisitiza juu ya Kilimo cha Kahawa hasa tunapoelekea kutekeleza Sera ya PESA KWA WOTE ifikapo Mwaka 2030 ambapo kupitia Kilimo cha Kahawa na Mazao mengine ya Matunda na Nafaka tunatarajia kila Mwananchi atakuwa na uwezo wa kumiliki zaidi ya Milioni 10 kupitia Uchumi wa Dhahabu Nyeusi (Kahawa, Mean Annum Per Capital Income ~ 10m).
Aidha, Mhe. Ndaisaba Ruhoro amewasisitiza Watu kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Mkaazi ili kuweza kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji.
Vilevile, Mhe. Ndaisaba Ruhoro amewakumbusha wanachi kubeba Miche ya Kahawa watakayoweza kuihudumia bila kusahau kuipatia huduma ya Maji Miche hiyo mara tu inapofika mwezi wa Sita mwezi wa Saba, wa Nane na wa Tisa mwanzoni ambapo ni miezi ya kiangazi ili kuepuka miche kukaushwa na Jua.
Mwisho, Mhe. Ndaisaba Ruhoro amewaomba maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika katika eneo hilo kwa kuwakumbusha waendelee kumuamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ifikapo 2025 wananchi wampigie Kura na kumchagua kwani ameleta maendeleo ya kweli kwa Wana Ngara na ili Kazi Iendelee zaidi.