Pre GE2025 Mbunge Nicodemus Maganga: Wilaya ya Mbogwe kuwa na mabadiliko makubwa ifikapo mwaka 2027

Pre GE2025 Mbunge Nicodemus Maganga: Wilaya ya Mbogwe kuwa na mabadiliko makubwa ifikapo mwaka 2027

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

GC51PySXsAAcBr3.jpg

Mbunge wa Mbogwe, Mhe. Nicodemus Maganga, amemshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa kufika Mbogwe kushiriki na wananchi katika Sherehe za kuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 na kuongeza kuwa Wilaya ya Mbogwe imejipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Madini kuendelea kufanya vizuri.

Mhe. Nicodemus Maganga Amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya nchini na kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo wilayani Mbogwe huku akiongeza kuwa, wanajipanga kuifanya wilaya ya Mbogwe kuwa yenye mabadiliko makubwa ifikapo mwaka 2027.

GC51O9kW8AAcOw2.jpg

Mhe. Nicodemus Maganga amesema hayo mbele ya wananchi wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita katika Sherehe za kuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 alizoziandaa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali mkoani Geita wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Martine Shigella.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko katika Sherehe za kuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 Amesema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia na Amewataka Wananchi kuchagua viongozi bora katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa

GC51O9mXIAAZeIk.jpg
 

Attachments

  • GC51PyaXEAAYIRu.jpg
    GC51PyaXEAAYIRu.jpg
    213.5 KB · Views: 6
Wanzuki haibadiliki kuwa Safari acheni laghai.
 
Uchawa mkubwa huu,fedha hazitoki kwa president, fedha za maendeleo zinatolewa na kuidhinishwa na bunge, na pia mtoa hoja elewa kuwa kikatiba hatuna wadhifa wa Naibu PM,,acha upumbavu
 
Back
Top Bottom