Mbunge Oliver Semguruka Aomba Serikali Kukamilisha Huduma za Afya Mkoa wa Kagera

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE OLIVER SEMGURUKA AIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA HUDUMA ZOTE ZA AFYA MKOA WA KAGERA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semguruka amechangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya Bungeni jijini Dodoma tarehe 15 Mei, 2023 iliyosomwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu

"Mkoa wa Kagera, Halmashauri sita zimekamilisha ujenzi wa Hospitali. Katoke Biharamulo, Bukoba DC, Bulembo Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara na Rusumo. Kuna Vituo vya Afya na Zahanati zimekamilika ila vinahitaji vifaa tiba" - Mhe. Oliver Semguruka

"Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya vimekamilika. Ninaiomba Serikali iweze kuleta vifaa tiba vya kutosha kwa ajili ya kutolea huduma za afya pamoja na Wataalam katika Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya" - Mhe. Oliver Semguruka

"Katika Hospitali na Vituo vya Afya vilivyokamilika tunahitaji ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya ili kuwezesha kutoa huduma kwa madaktari bingwa kwa masaa 24 ili kupunguza vifo vya mama wajawazito, watoto na wazee kutokana na ukaribu wa madaktari katika maeneo ya kazi" - Mhe. Oliver Semguruka

"Mkoa wa Kagera katika mipaka kuna mapungufu makubwa katika kupunguza magonjwa hatarishi. Tunaomba kujengewa majengo ya Medical Department na Isolation ili huduma katika mipaka yetu ya Mtukula, Chamchuzi, Bugango, Mrusagamba, Igoma, Rusumo na Kabanga ili kudhibiti magonjwa hatarishi" - Mhe. Oliver Semguruka

"Mkoa wa Kagera upo katika mlipuko wa majanga mengi, tunahitaji kujengewa kituo cha ufuatiliaji wa matukio ya mlipuko kwa mfano Ebora, Marburg, Surua, Polio, Yellow fever na UVIKO-19 kwa sababu tumepakana na mipaka ya nchi jirani na tunaomba Serikali ituangalie kwa jicho la huruma" - Mhe. Oliver Semguruka

"Mkoa wa Kagera tuna visiwa 38. Visiwa 5 tu ndiyo vina Zahanati. Mama wajawazito visiwani hawana mahali pa kujifungulia. Ili kunusuru uhai wao tunaomba Serikali itununulie Ambulance 🚑 ili kuwezesha dharura za matibabu kutoka kwenda visiwa vingine" - Mhe. Oliver Semguruka

"Mkoa wa Kagera umeanza upanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kubomoa majengo chakavu na sasa hivi tumeanza kujenga maghorofa. Tuliahidiwa kuletewa Bilioni 3 ili kuweza kumalizia. Tunaomba fedha ije kipindi hiki ili tuendelee na ujenzi wa OPD, Wodi za watoto na Wodi za Wanawake" - Mhe. Oliver Semguruka

Your browser is not able to display this video.
 
Huyu Mheshimiwa Semguruka kweli anaonyesha uchungu kwa maendeleo ya wana Kagera. Hopitali ya Rufaa kwa sasa haina hadhi na viwango vya ubora ikilinganishwa na changamoto za kiafya zinazoukabili mkoa huu.

Hebu linganisha hospitali ya mtwara na kagera mkoa unaopakana na nchi 3 tena ng'ambo ya ziwa kubwa ktk bara la afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…