Mbunge Priscus Tarimo alaani tukio la Idrisa Makishe kumwagiwa tindikali

Mbunge Priscus Tarimo alaani tukio la Idrisa Makishe kumwagiwa tindikali

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini(ccm),Priscus Tarimo amelaani tukio la kada wa chama hicho ,Idrisa Moses Makishe(38),kumwagiwa kimiminika kinachoaminika kuwa ni tindika.

Makishe kada wa ccm ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa kwa viongozi wa ccm ambao wamekuwa hawaendani na falsafa ya chama hicho,alikumbwa na mkasa huo septemba 20 mwaka huu majra ya saa mbili usiku.

Makishe ambaye ni mwendesha bodaboda kwenye kituo cha Kizotw kata ya Bonden,alikodiwa na mtu mmja akitaka ampeleke eneo la Njoro Relini.

Abiria huyo alipofika njiani aliomba asimame Ili amchukue mwenzake .

Hapo ndipo alipojitokeza mtu ambaye alimwagia kimiminika hicho na wawili hao kuondoka na pikipiki yake aina ya Sonorai MC 854 DCB.

Makishe alikimbizwa Hospital ya Rufaa ya mkoa,Mawenzi kwa matibabu kabla ya kuhamishiwa Hospital ya Rufaa ya Kanda,KCMC ambako anaendelea na matibabu mpaka sasa.

Kufuatia tukio hilo,Mbunge Priscus Tarimo aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kulaani tukio hilo .

" Ninalaani kwa nguvu zote tukio hili.",ameandika Priscus na kuendelea

"Idrisa Makishe jana jioni(septemba 20) amekodiwa kutoka kituo cha bodaboda cha Kizota Kata ya Bondeni, kumpeleka abiria Njoro "

"Na kwa bahati mbaya abiria wake na mtu mwingine aliyekuwa anasubiri kwenye eneo alilotaka kupelekwa abiria kwenye Kata ya Njoro, walimvamia, kumpiga na nyundo kichwani, kumwagia kimiminika kinachoaminika kuwa tindikali usoni na sehemu nyingine za mwili na kisha kuondoka na pikipiki yake kuu kuu"

"Wahusika walitaka lionekane kama tukio la unyang’anyi au uporaji lakini kwa muonekano wa awali kuna mazingira ya udhalimu wa kisiasa"

"Ninamtakia uponyaji wa haraka na wa uhakika ndugu yetu Idrisa Makishe wakati tukisubiri taarifa zaidi kutoka kwenye vyombo husika",amemalizia .

Hili ni tukio pili mkoani Killimanjaro kwa watu kumwagiwa Tindikali ambako machi 5 mwaka 2020,Tariq Kipemba naye alikumbwa na mkasa huo NYAKATI za saa mbili usiku eneo la Shanty Town mjini moshi .

Tariq kwa sasa amepoteza jicho moja kutokana na mkasa huo na kufuta kabisa ndiyo zake za kujikwamua kimaisha.

Tuviachie vyombo vya dola vifanyekazi yake Ili kuona haki ya Makishe na Tariq inapatikana .


Haya ni maneno ya mbunge wa Jimbo la Moshi mjini,Priscus Tarimo septemba 21,2024 kupitia akaunti yake ya Facebook baada ya tukio la Idrisa Makishe kumwagiwa Tindikali

Naomba yaongezwe kwenye story yetu

Pia soma
- Kada wa CCM amwagiwa tindikali
 
Back
Top Bottom