Mbunge Robert Kyagulanyi 'Bobi Wine' aachiwa kwa dhamana na kutakiwa kukabidhi hati yake ya kusafiria

Mbunge Robert Kyagulanyi 'Bobi Wine' aachiwa kwa dhamana na kutakiwa kukabidhi hati yake ya kusafiria

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mwanamuziki mwanasiasa Bobi Wine ambaye amekuwa akizuiliwa kwa karibu wiki mbili nchini Uganda ameachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu, kaskazini mwa nchi hiyo.

Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi amepewa dhamana pamoja na wabunge wengine watatu, na watuhumiwa wengine wanane.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kurushia mawe magari ya msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Arua.

Kassiano Wadri aliyeshinda ubunge Arua ni miongoni mwa wabunge waliokuwazuiliwa.

Bw Wadri ameachiliwa kwa dhamana lakini akazuiwa kuzuru eneo bunge lake kwa miezi mitatu bila idhini ya mahakama.

Maombi ya dhamana ya washukiwa wengine 21 walioshtakiwa pamoja na Bobi Wine yatasikilizwa na mahakama baadaye leo.

Awali, taarifa zilikuwa zimesema kuwa wakili wa kimataifa aliyekuwa amepewa kazi ya kumwakilisha, Bobi Wine, amezuiwa kuingia nchini humo.

Gazeti la kibinafsi la the Monitor nchini humo limeripoti kuwa Robert Amsterdam ameorodheshwa kama mtu asiyetakikana nchini Uganda na serikali ya nchi hiyo.

Alikuwa miongoni mwa mawakili waliokuwa wameorodheshwa kumtetea Bw Kyagulanyi katika kesi ambapo ameshtakiwa uhaini.

Gazeti la kibinafsi la the Monitor nchini humo limeripoti kuwa Robert Amsterdam ameorodheshwa kama mtu asiyetakikana nchini Uganda na serikali ya nchi hiyo
 
The guy is gonna be a president..one day

Ugiligili
 
Mwanamuziki maarufu nchini Uganda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyadondo, Bobi Wine ameachiwa huru kwa dhamana leo Agosti 27, 2018 na Mahakama Kuu mjini Gulu.

Bobi Wine
Robert Kyagulanyi a.k.a Bobi Wine amekuwa akizuiliwa na jeshi la polisi kwa takribani wiki mbili nchini humo amepewa dhamana pamoja na wabunge wenzake watatu, akiwemo Mbunge mteule wa jimbo la Arua.

Kwa upande mwingine Mahakama hiyo pia, imewaachia watuhumiwa nane kwa dhamana, wote wanadaiwa kuhusika kurushia mawe msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arua.

Hata hivyo, wakati watu wakifurahia dhamana hiyo, Bobi kwenye video zake zinasombaa mtandaoni anaonekana hajapona kwani anashindwa kusimama mpaka sasa.

DlmRqJEW0AAX1nn.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi viongozi wa kiafrika hawajifunzi tu walikuwepo wababe kama wakina c.tylor na wengineo lkn mpaka leo mwisho wao ni mmbaya

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom