Mbunge Rose Tweve Asema Hajaridhishwa na Majibu ya Serikali

Mbunge Rose Tweve Asema Hajaridhishwa na Majibu ya Serikali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
📌 AHOJI UTEKELEZWAJI WA AAGIZO LA WAZIRI MKUU

📌 ATAKA KUJUA HALI YA KIUTENDAJI KWENYE HALMASHAURI ILIVYO

MBUNGE wa Viti maalum Mkoani Iringa Mhe. Rose Tweve ametaka kujua kiundani juu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliliolitowa mapema tarehe 22 Mei 2024 akiziagiza Halmashauri kuu zote Nchini kutenga Bajeti juu ya ununuzi Dawa za kupambana na Mbu huko Kibaha.

Mhe. Rose Tweve akizungumza mbele ya Naibu spika wa Bunge amesema "Mhe. Naibu Spika bado sijiridhishwa na majibu ya Serikali, Swali langu lilikuwa wazi kuwa ni Halmashauri ngapi hapa Nchini zimetekeleza agizo la waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizitaka Halmashauri Kuu Nchini kutenga Bajeti juu ya ununuzi wa Dawa Kibaha na kusambaza kwenye Halmashauri zote Nchini katika kuhakikisha wananyunyuzia mazalia ya mbu ili kuokoa maisha ya Watanzania wakiwemo akina mama na watoto".

Aidha, Mhe. Rose Tweve ameisisitiza Serikali kuchukua hatua za haraka katika kutekeleza agizo hilo la Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa

#Alamaonline #Pamojatuongee

 
Back
Top Bottom