Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro pamoja na uongozi wa CCM Wilaya na kata pamoja na MH.BURINDORI diwani wa Kibogora wameshiriki zoezi la kuwashwa Kwa Mnara katika Kijiji Cha Mururama kata ya Kibogora wilayani NGARA.
Uwashwaji wa mnara huo unahitimisha ahadi aliyoitoa MH.RUHORO katika kipindi cha uchaguzi mwaka 2020 ya kuhakikisha kata ya Kibogora inapata huduma ya mawasiliano ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Wakati akizungumza na wananchi MH.RUHORO amempongeza DR SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kutimiza ahadi hiyo na amewaomba wananchi kumchagua kwa KISHINDO DR SAMIA SULUHU HASSAN kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.
Wananchi walionyesha mapenzi makubwa Kwa Mbunge na kuahidi kumuunga mkono na kumuombea mafanikio katika shughuri zake.