Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Saashisha Mafuwe akabidhi mashine ya X-ray yenye thamani ya Tsh. milioni 196 na magari mawili
Your browser is not able to display this video.
Mbunge wa Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro, Saashisha Mafuwe tarehe 10 Agosti, 2024 amefanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Hai na kukabidhi Ultrasound na X Ray Machine za kisasa zenye thamani ya zaidi ya Milioni 196 pamoja na Magari Mawili ya Hospitali ya Wilaya.
Saashisha Mafuwe ametembelea na kuona vifaa na majengo mapya ikiwemo; Jengo la wodi ya wazazi, Jengo la Maabara, Jengo la Famasi, Jengo la Private ward, Njia za kuunganisha majengo yaani walk way, Jengo la incinerator yaani machine ya kuchoma taka, Jengo la ICU.
Zaidi ya Wananchi 350 ambao hufika kupata matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Hai kila siku wanatarajia kunufaika na huduma bora za kiafya zitolewazo hospitalini hapo baada ya Serikali kuendelea kuboresha huduma hizo ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba mbalimbali.
Soma Pia:
- Mbunge wa Nkenge, Florent Kyombo akabidhi kompyuta
- Mbunge Tauhida akabidhi Vifaa vya Ofisi Shule za Kijitoupele na Bububu
"Leo hii tuna X -ray Mashine mpya, ICU yenye vifaa vyote vya kisasa, maabara pamoja na wataalam wa kutosha, hakika hii ni dhamira nzuri ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutuhudumia wananchi wa Hai" - Saashisha Mafuwe.