LGE2024 Mbunge Samizi achanja mbuga kunadi Wagombea wa CCM Muhambwe

LGE2024 Mbunge Samizi achanja mbuga kunadi Wagombea wa CCM Muhambwe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
MBUNGE SAMIZI ACHANJA MBUGA KUNADI WAGOMBEA WA CCM MUHAMBWE.

Apita mguu kwa mguu Kata za Mkabuye, Rugongwe, Busagara kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo.

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Dkt. Florence George Samizi ameendelea kuchanja mbuga kuwaombea kura na kuwanadi wagombea wa CCM ambapo wikendi hii Jumamosi na Jumapili amezitumia ipasavyo kwenye Kata za Mkabuye, Rugongwe na Busagara akifanya Mikutano ya Kampeni akiwaombea kura na kutoa sera za CCM na kuwaambia mambo ambayo tayari serikali ya CCM iliyoyafanya katika Kata hiyo hizo na ambayo inatarajia kuyafanya, hususani Ujenzi wa Zahanati ya Nyakilenda, Shule ya Secondari ambayo tayari ilishakamirika ambayo ilikuwa hitaji kubwa la wananchi wa Kata ya Mkabuye ikiwa Watoto walikuwa wanahangaika kuifuata Shule ya Secondari ITABA iliyopo umbali wa Km 10.

Ambapo amewaomba wananchi na wanachama wote waliojiandikisha kwenye Daftari la mkaazi wajitokeze Tarehe 27 November 2024 kuwapigia kura za ndio Wagombea wa Chama cha Mapinduzi, akisisitiza wananchi wasipuuze kwenda kupiga kura kwa wagombea ambao hawana wapizani eti walishapita bila kupingwa wakati itapigwa kura ya ndio na hapana.

Pia, Mbunge Dkt. Samizi amefanya Mikutano ya hadhara ya Kampeni katika Kata mbili za Rugongwe na Busagara akiendelea kusisitiza wananchi wa Kata hizo kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wote wenye sifa za kupiga kura wanajitokeza kupiga kura kwa wagombea wa CCM.

Aidha, Dkt. Samizi amewataka viongozi wote ambao watapata nafasi hizo za kuwatumikia wananchi wahakikishe wanakuwa watumishi wa wananchi na sio miungu watu na kuwasahau waliowapa heshima.

Amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inahitaji Viongozi wawajibikaji, Wazalendo, Waadilifu na wenye hofu ya Mungu ya kuwaongoza wananchi kwa weledi.

Lengo Kuu la Mbunge; Dkt. Florence Samizi ni kulitaka Jimbo la Muhambwe kupambwa la kishindo Kwa rangi ya Kijani tu katika Vijiji na Vitongoji vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

IMG-20241125-WA0060.jpg
IMG-20241125-WA0056.jpg
IMG-20241125-WA0058.jpg
IMG-20241125-WA0052.jpg
IMG-20241125-WA0054.jpg
IMG-20241125-WA0046.jpg
IMG-20241125-WA0050.jpg
IMG-20241125-WA0048.jpg
IMG-20241125-WA0044.jpg
IMG-20241125-WA0042.jpg
 
Back
Top Bottom