BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Atumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu
Katika harakati za kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan anayepambana kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuenenda na Mpango wa Taifa wa utunzaji wa mazingira kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi ameweza kugawa takribani mitungi 200 kwa Mama na Baba lishe.
Hii ni sehemu ya uungwaji mkono wa kampeni ya Taifa chini Rais Samia Suluhu Hassan ambapo zipo faida chanya nyingi za utumiaji wa Nishati Safi ya Kupikia ukilinganisha na utumiaji wa kuni na mkaa.
Utumiaji wa Nishati Safi ya Kupikia kama gesi hupunguza uzalishaji wa Gesi ya ukaa ambayo ni mbaya kiafya, kuokoa misitu, kulinda afya kwani majiko yanayotumia nishati safi hupunguza moshi hatari unaotokana na kuni au mkaa, ambao huathiri afya ya binadamu, hususan magonjwa ya kupumua.
Soma Pia:
~ Bashungwa Agawa Mitungi ya Gesi 300 kwa Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum
~ Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025