Mbunge Samizi asimama bungeni kupigania ujenzi skimu ya nyendara, serikali yatoa majibu
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence Samizi Ijumaa Februari 07, 2025 amesimama Bungeni kuiulizia Serikali kuhusu ukamilishaji wa Skimu ya Nyendara.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde amemjibu Mhe. Mbunge Samizi kwa niaba ya wananchi wa Muhambwe kwamba Serikali iko tayali kuijenga na taratibu za upembuzi yakinifu kuelekea kuijenga zimeshafanyika.