BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Mhe. Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe amekua Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa kuelekea maadhimisho ya kumi na moja {11 ya siku ya Wanyamapori Duniani ambayo kitaifa yanafanyika leo Tarehe 3 Machi 2025, Kitaifa Jijini Dodoma.
Uzinduzi huo umefanyika shule ya sekondari Muhambwe ikiwa na lengo la kuungana na Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusherekea siku ya Wanyamapori Duniani. Maadhimisho ya mwaka huu 2025 Kitaifa yanafanyika Jiji la Dodoma na kimkoa yamezinduliwa katika Wilaya ya Kibondo siku ya 27 Februari 2025 yakiongozwa na kauli mbiu inayosema "fedha za Uhifadhi wa Wanyamapori kuwekeza kwa watu na mgeni rasmi akiwa Mbunge Samizi.
Shughuli ambazo zimefanyika ni upandaji wa miti ya matunda ya parachichi pamoja na miti ya kivuli ambapo Mbunge Samizi amewasisitiza kuitunza miti hii ambayo imeandaliwa kwa gharama kubwa.
Mara baada ya shughuli za kupanda miti, Mbunge Samizi alizungumza na wanafunzi na kuwapa million moja taslimu na kuwaahidi kuwapatia jezi pea 4 ndani ya siku za hivi karibuni.
#Samizi na Muhambwe 2025-2030.
Imetolewa Na;
Kitengo cha habari na mawasiliano Ofisi ya Mbunge Jimbo la Muhambwe.