JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mbunge wa Makete Festo Sanga ameitaka serikali kuangalia upya bei ya tiketi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania kwa kuwa ni kubwa kulinganisha na uhalisia."
Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Mapango wa Taifa.
Sanga amesema: "Ukikata tiketi ya DSM kwenda Katavi ni sawa na kukata tiketi ya kwenda nje ya nchi, bei hizi zinakatisha tamaa kwa Watanzania kutumia usafiri wa ndege kwenye kuharakisha shughuli zao za kiuchumi.
"Nchi hii imewahi shuhudia shirika la ndege binafsi la Fast Jet likirusha Air Bus kutoka DSM kwenda Mwanza na maeneo mengine kwa bei ya chini sanaa ambayo Watanzania wengi walifurahia kusafiri na usafiri wa ndege.
"Sasa hizi za Air Tanzania ni ndege zetu Watanzania, viwanja ni vyetu kwanini bei zipo juu sana? Naomba serikali ilitazame hili kwa maslahi mapana ya nchi yetu". amesema Sanga</p>
Akizungumzia uboreshaji wa viwanja vya ndege, Sanga amesema: "Air Tanzania inakwama kuruka usiku kwasababu viwanja kadhaaa kama Kigoma, Dodoma, Tabora, Bukoba n.k havina taa za kusaidia ndege kuruka usiku.
"Tunapokwenda kulala na zenyewe zinalala, hili jambo linakwamisha sanaa, ni vyema ATCL ikaruka zaidi usiku kuliko mchana muda wa kazi, hivyo TAA (Tanzania Aviation Authority) iboreshe viwanja kwa kuweka taa na kuongeza Control Tower kwenye viwanja vya ndege hasa pale Bukoba ambako wanatumia control Tower ya Mwanza," amesema.
Chanzo: IPP