Mbunge Santiel Kirumba agawa Mitungi ya Gesi 200 kwa Wakunga wa Shinyanga DC na Manispaa

Mbunge Santiel Kirumba agawa Mitungi ya Gesi 200 kwa Wakunga wa Shinyanga DC na Manispaa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Eric Kirumba mnamo tarehe 9/7/2024 alishiriki kugawa Mitungi ya Gesi kwa Wakunga wa Shinyanga DC na Shinyanga Manispaa kuwahamasisha kutumia nishati mbadala

"Tunatambua majukumu waliyonayo Wakunga, ili kutimiza majukumu yao kwa haraka tuliona tuwapatie nishati ya gesi ambayo itawasadia kuwahamisha Mama wajamzito waweze kutumia gesi maana moshi wa mkaa na kuni huathiri mapafu na takribani watu 75,000 hufariki kwasababu ya matumizi ya moshi" - Mhe. Santiel Eric Kirumba

Clean Cooking Campaign iluzinduliwa kitaifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika harakati za kumtua kuni mwanamke kichwani na kutunza mazingira ili kujiepusha na mabadiliko ya tabianchi

"Nawashukuru, Doris Mollel, Doris Mollel Foundation (DMF), Oryx Energies Tanzania kwa kuweza kufanikisha hili kwa Mkoa Shinyanga na Campaign hii ya Clean Cooking kwa watumishi wa Sekta ya Afya ambapo tuligawa mitungi 200" - Mhe. Santiel Eric Kirumba.

WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.01.59.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.00.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.01(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.02(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.02.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.06.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-10 at 21.02.07.jpeg
 
Back
Top Bottom