Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE SANTIEL KIRUMBA Aitaka Serikali Kuiongezea ROAD FUND Bajeti ya Kutosha Ili Kuboresha Barabara (KM 71) Kongwe Nchini
"Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa jinsi alivyoweza kununua mitambo ya kisasa ya TMA na kupelekea TANROAD kufanya kazi kwa ufasaha kipindi cha Elnino ilivyotokea nchini, la sivyo isingekuwa rahisi kugundua kuwa kuna Mvua kubwa sana zinakuj" - Mhe. Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga
"Mheshimiwa Rais alitoa Fedha ya Dharua (Emergency Fund) Shilingi Bilioni 6 kwenda kutatua matatizo ya mitandao ya Barabara iliyokwama. Mkoa wa Shinyanga ni wanufaika namba moja ambao tulipata Shilingi Bilioni 1.9. Mheshimiwa Rais amekuwa macho kuhakikisha Tanzania haisimami maana Barabara ni siasa na uchumi" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Mheshimiwa Rais alihakikisha anatekeleza miradi aliyoikuta. Tuna kauli yetu mbiu tunasema HAKUNA KILICHOSIMAMA Hakuna Kijiji ambacho hakijafikiwa, Mheshimiwa Rais ni mchapakazi na ana maono makubwa sana na Wizara ya Ujenzi, pia amewaweka na kuwaamini vijana" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Nampongeza Meneja wa TANROAD Mkoa wa Shinyanga, Eng. Joel. Ameshirikiana vizuri kuhakikisha Barabara zinapitika, madaraja yanaungana, njia zinapitika na tunaendelea na shughuli za kiuchumi. DC Mboni amefanya kazi kubwa sana, apokee Maua yake katika Mkoa wa Shinyanga" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Bunge lililopita nilisema, Road Fund kwa mwaka inahitaji Shilingi Trilioni Moja lakini kwa mwaka Serikali Kuu inaipelekea Shilingi Bilioni 600. Ni kitu hakiwezekani, vyanzo vya mapato ya Road Fund ni vichache kuweza kuhudumia mtandao mkubwa wa Barabara 71 Tanzania nzima" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Tutailaumu sana Serikali na Waziri wa Ujenzi bila kufikiri kuwa Serikali imefika mahali imebanana. Namuomb Waziri wa Fedha aangalie chanzo kipya cha kuisaidia Road Fund kupata Shilingi Trilioni Moja kwa mwaka. Barabara ya Dodoma - Morogoro - Dar es Salaam imejaa viraka ina mashimo mengi" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Tumekuwa tukisaini Barabara mpya kila kukicha, Barabara kongwe hazipitiki. Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari walisema Laini za Simu ambazo ni Active ni Milioni 72, kama kila Laini tulipata labda Shilingi 50 ili iweze kuisaidia Road Fund" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Suala la fidia ni changamoto, mpaka sasa Serikali inadaiwa Shilingi Trilioni 7. Kiwanja cha Ndege cha Ibadakui, Shinyanga kilitathiminiwa mwaka 2017, Kaya 80 zimelipwa Aprili 2024 Shilingi Milioni 320" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Fikiria, mwananchi anajitolea ardhi yake kuipisha Serikali kufanya mradi na Serikali inachelewa kumlipa mwananchi. Wananchi ni wa hali ya chini, kutafuta kiwanja ni Shilingi Milioni Moja. Kama Serikali hamna miradi ya haraka na hamna fedha muwaache wananchi wakae" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Unatumia miaka 7-8 kumlipa mwananchi, Serikali mnavyolimbikiza fidia ni hasara kwa Serikali, ni hasara kwa Wananchi maana mnavyolimbikiza gharama za fidia zinapanda na gharama za vifaa zinapanda mwaka hadi mwaka" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Kama Serikali haijajipanga kuwalipa fidia wananchi, msiwawekee wananchi X, muwaache wananchi wakae waendelee na shughuli zao. Mtakapokuwa tayari muwalipe fidia kwa wakati" - Mhe. Santiel Eric Kirumba
"Madeni ya Wakandarasi ni changamoto, tunakoelekea Mabenki itakuwa ni shida. Invoice discount ndani ya masaa 24, Shilingi Bilioni 900 ziko nje, mwaka 2025 zitakaribia Trilioni, Serikali haijaweza kulipa, Madeni yana riba. Bilioni 44 ni riba. Serikali inaingia kwenye hasara" - Mhe. Santiel Eric Kirumba