Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SEBASTIAN KAPUFI ATAKA KASI IONGEZEKE UJENZI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI MPANDA
"Je, Serikali inasema nini kuhusu kasi ndogo ya mradi wa Umwagiliaji Kata ya Mwamkulu Mpanda" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
"Mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji iliamza utekelezaji wa mradi wa Umwagiliaji Mwamkulu ambao ulisuasua awali kutokana na kuchelewa kwa malipo ya Awali ya Mkandarasi. Kwasasa Malipo yamekamilika na kazi ya ujenzi inaendelea na utekelezaji wake umefikia 50%" - Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde
"Je, Serikali inayotaarifa kuwa kasi bado ni ndogo na kusuasua kwa awali kumerejea tena? Msimu wa Mvua umeanza na Wananchi wanalitegemea Bonde hilo kupitia Skimu ya Kienyeji. Serikali inawasaidiaje Wakulima wakati mradi haujaanza?" - Mhe. Sebastian Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
"Mkandarasi bado yupo ndani ya muda maana mradi unatarajiwa kukamilika Aprili 2025 na tumeshapeleka fedha. Pia huwa tunawaruhusu Wakulima msimu wa Mvua kutumia Bonde bila kuathiri miundombinu ambayo Mkandarasi anaitengeneza" - David Silinde