Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Simon Kapufi wakati akiwaombea kura katika Kampeni wagombea wanaotokana na CCM amewashukuru Wananchi wa Mpanda Mjini kwa kuwaamini wagombea wa CCM kwani inaonyesha wanakubalika katika maeneo yao.
"Wananchi wote itakapofika tarehe 27 Novemba, 2024 mkapige kura mturudishie viongozi watakaoendelea kusimamia maendeleo kutokana na fedha nyingi za miradi zilizoletwa kwani Chama Cha Mapinduzi kimefanya mambo mengi mazuri kwa Wananchi" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini.
Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sebastian Simon Kapufi ameainisha miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ikiwemo miradi ya Elimu, Afya, Miundombinu ya Barabara na Madaraja, Kilimo, Madini, Biashara ambayo kwa kiasi kikubwa imebadirisha mandhari ya Mpanda Mjini tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Mhe. Kapufi amewasihi sana wananchi Jimboni Mpanda Mjini kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi tarehe 27 Novemba 2024 ili kuendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameonyesha nia ya dhati kwa kuwatumikia wananchi wote.