Mbunge Sebastian Kapufi Katika Mafunzo ya Kamati ya Bunge ya TAMISEMI Yaliyoendeshwa na PPPC

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

KITUO cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Simon Kapufi amezungumza na kuchangia mada wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya PPPC ambayo yamefanyika Novemba 11, 2024 katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.


Katika mambo ambayo yamejadiliwa ni pamoja umuhimu wa kutumia PPP katika utekelezaji wa Mipango ya Taifa ya Maendeleo ya nchi, muundo wa kisheria na Kitaasisi katika utekelezaji wa program ya PPP Tanzania.

Mambo mengine ambayo yamejadiliwa ni pamoja na dhana ya PPP na Orodha ya Miradi ya PPP iliyoandaliwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa


 

Attachments

  • GcH4RVTWwAAqO02.jpg
    316.4 KB · Views: 6
  • GcH4RVLWoAAarhP.jpg
    419.8 KB · Views: 5
  • GcH4SlcWMAAv7bM.jpg
    356.6 KB · Views: 5
Maamuzi ya hiyo mijadala ni yapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…