Tujaribu kupitia orodha za ajali za wabunge wa CCM, na hatua zilizochukuliwa dhidi yao. Yule dereva wa Chacha Wangwe (CHADEMA) alitumikia kifungo, huyu Selasini anashtakiwa, Regia (R.I.P) alifariki, sasa tuangalie madereva wa Kapuya, Salome Mbatia, Mudhihir, Menrad Kigola, Mussa Khamis Silima (alikuwa akiendesha yeye, mkewe akafa) na wengine wengi wa CCM
Ssa angefanyaje?kama tairi limepasuka?Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limesema litamfikisha mahakamani Mbunge wa Jimbo la Rombo, (Chadema), Joseph Selasini (50), kufuatia ajali ya gari alilokuwa akiendesha kusababisha vifo vya watu wanne.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, ambaye kwa sasa amehamishiwa mkoani Mara, aliieleza hayo NIPASHE Jumamosi, kuhusu hatua zinazofuata baada ya ajali hiyo ambapo mbunge huyo alikuwa dereva wa gari hilo.
Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani, dereva anayesababisha ajali hufikishwa mbele ya chombo cha haki ambacho ni mahakama.
Alisema wanachosubiri ni michoro ya askari aliyepima ajali hiyo, kwani yapo mambo mengi kutokana na ajali hiyo iliyotokea katika barabara kuu ya Moshi Arusha baada ya gurudumu kupasuka.
Polisi tuna maadili, tunasubiri apone kwani alikuwa mahututi na amefiwa na mama yake mzazi, mkwe na ndugu wengine huku mke wake akiwa bado yu mahututi hospitalini, tutapima ajali na tutachunguza...Sheria lazima ifuate mkondo wake na kesi dhidi yake ipo pale pale, alisema Mwakyoma.
Aidha, alisema ajali hiyo inahitaji uchunguzi wa kina kwa kuwa inahusisha mambo mengi ikiwemo gurudumu moja kupasuka na kisha gari kwenda kuparamia kalavati, hivyo mara baada ya uchunguzi kukamilika sheria itafuata mkondo wake.
Ajali hiyo ilitokea Mei 24, mwaka huu, majira ya saa 1 usiku, katika eneo la Chuo cha Ufundi Bomangombe, barabara ya Moshi Arusha, wakati akitokea kwenye msiba wa padri mkoani Arusha, ambapo watu wawili walifariki papo hapo.
Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa ni mwendo kasi na kumkwepa mwendesha pikipiki. Gari lilikuwa likiendeshwa na mbunge huyo ni lenye namba za usajili T 441 BRT aina ya Toyota Land Cruiser VXR s/Wagon.
Katika gari hilo, kulikuwa na abiria sita, ambapo wawili walifariki eneo la tukio, mmoja hospitali ya wilaya ya Hai, na mwingine usiku baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge huyo, aliiomba Serikali kufanya ukaguzi wa kina wa bidhaa na vipuri vya magari vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi, kwa kuwa ni siku tatu zilizopita alinunua magurudumu ya gari hilo, ikiwa ni pamoja na elimu kwa waendesha bodaboda na baiskeli.
Hii ni ajali ya pili kwa mbunge huyo, baada ya ajali ya kwanza mwaka juzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, ambapo alivunjika mkono wa kulia mara tatu.
Sosi: ippmedia.com
Eti police wana maadili! Wangekuwa na maadili wangeuwa raia wasiokuwa na hatia? Wangekuwa wakijizolea rushwa kila kukicha!?
Usijekuta huyu mchaga hata hela anayolipwa kama mshahara wa dereva anameza.
duh!hivi ndugu tayari ishathibitishwa beyond reasonable doubt kwamba ajali ilitokana na uzembe wake?mbona watu wengine mnapenda kukurupukia sana mambo?anyway,pole zake na wote walopatwa na misiba kutokana na ajali hiyo.ni matumaini yetu kuwa polisi watakuja na sababu za 'kitaalam' za chanzo cha ajali hiyo....ili in kuwa funzo la kuepuka kutokea tena kwa ajali za dizaini hiyo...!
haya ndio matatizo ya ndugu zangu wachaga,badiliken ndugu zangu! Hela zote anataka yeye, looh!!!
God must love crazy people because he make so many of them....wewe utakuwa lichaga,kwa kubebana nyie,mnatisha! Uzalendo kwenu ni ukabila.
Hili nalo Litapita
Huyu mbunge anaonekana ni careless sana haiwezekani ukawa na ajali mbili mpigo, na inasemekana anaendesha kwa fujo sana haya magari ya mkopo.
Well, kama alimpenda Mama yake mbona yeye alifunga mkanda lakini Mama yake hakumfungisha?....ni mtu gani aliye normal asiyempenda mama yake mzazi na kumjali"
Kila siku ajali zikitokea utasikia matairi yamepasuka, matairi yamepasuka, matairi yamepasuka, uongo mtupu, mbona nchi zilizoendelea husikii kila siku matairi yamepasuka?Ssa angefanyaje?kama tairi limepasuka?
mkuu, taratibu basi. unachopinga ni mbunge kushtakiwa au ni nini? kama we ni dereva, nadhani unajua sheria ya usalama barabarani, lkn kama ni layman na hujishughulishi kujisomea ndo mwanzo wa kauli kama zako. Ajali imetokea, na kupelekwa mahakani ndiko kuitafuta hakiaskari wetu ni maffaa*** la kweli .. Badala ya kupiga vita ili serikali iache kuingiza bidhaa fake hasa kutokea kenya wanakuja na mashairi ya ajabu ajabu hapa.. Sishangai kuwa wengi wao wana vyeti fake.
kuna tangazo la kondomu linasema, " kama kweli unampenda utamlinda". kama alimpenda mama yake na wote waliokuwa ndani ya gari, mwenda kasi wa nini? kwani alikuwa marathon? haya kuna safety rules kwa wapanda magari, alizingatia? mfano kufunga mikanda na mengine? halafu yeye ni mheshimiwa, na tayari analipwa hadi hela ya dereva, kwa nini aendeshe yeye? kama siyo uchu na dhuluma vimemtawala ni nini? kwenda mahakaman aende ili pia mambo mengine yarekebishwe. na tusipofanya hivyo, ipo siku na rais wa jamhuru atachukuwa benzi za ikulu aanze kuendesha mwenyewendugu mpendwa,ninakushauri utafute kamusi ya kiswahili na utafute maana ya neno ajali.kisha nenda katafute kamusi kiingereza(dictionary) tafuta tena maana ya neno ajali(accident).baada ya kusoma kwa umakini,nenda kwenye google tafuta maana ya neno "RISK".baada ya kufanya zoezi hilo jepesi,kaa utafakari haya;"ni mtu gani aliye normal asiyempenda mama yake mzazi na kumjali"."je sisi binadamu ndio huwa tunapanga ni wakati gani tuugue na ni wakati gani tuwe na siha njema?"fikiriri kabla ya................