Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliver Semuguruka amefanya Kitendo cha Utu, huruma na mfano mzuri wa kuigwa baada ya kuamua kumlipia deni mkazi mmoja wa Mkoa wa Iringa aliyekumbiwa na mke wake kwasababu ya madeni ya Brac.
"Mke amekimbia ameniachia watoto, tulishauriana aende achukue mkopo ili tupate uwanja cha Tsh 300,000 au Tsh 400,000 ambapo marejesho ilikuwa kama Shilingi 15,000 kwa wiki lakini yeye alivyoenda alichukua 1,200,000 ambayo kwa wiki ni marejesho ya shilingi 38,000 ambayo nashindwa kuifikisha" - Mkazi wa Iringa (Mdaiwa)
"Walishachukua Sabufa, TV, na vitu vingine vimeisha. Mpaka sasa tumebaki na Sofa moja tu ambapo Brac wamesema watakuja kumalizia na Masufuria. Kazi yangu ni kubonda Kokoto ambayo Ndoo moja ni 1,000" - Mdaiwa, Mkoa wa Iringa.
"Kitendo hicho kilimuumiza sana kama Mama (tukiacha uanasiasa pembeni) nina hofu ya Mungu lakini pia kama mama nilijiuliza hawa watoto wangekuwa ni wa kwangu jinsi baba amewakumbatia katika shida, hakuamua kuwaacha" - Mhe. Oliver Semuguruka
"Nilimwambia yule Mzee nitamsaidia kulipa deni la kiasi kilichobaki. Nilimuambia Mwandishi wa Habari aende kwa yule mzee waende wanapodaiwa wapigiane mahesabu kisha aniletee Bili nimlipie"
"Niwasihi akina Mama, tuache tamaa ya kuchukua mikopo ambayo hatuwezi kuilipia" - Mhe. Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera