Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliver Semuguruka amefanya Kitendo cha Utu, huruma na mfano mzuri wa kuigwa baada ya kuamua kumlipia deni mkazi mmoja wa Mkoa wa Iringa aliyekumbiwa na mke wake kwasababu ya madeni ya Brac.
"Mke amekimbia ameniachia watoto, tulishauriana aende achukue mkopo ili tupate uwanja cha Tsh 300,000 au Tsh 400,000 ambapo marejesho ilikuwa kama Shilingi 15,000 kwa wiki lakini yeye alivyoenda alichukua 1,200,000 ambayo kwa wiki ni marejesho ya shilingi 38,000 ambayo nashindwa kuifikisha" - Mkazi wa Iringa (Mdaiwa)
"Walishachukua Sabufa, TV, na vitu vingine vimeisha. Mpaka sasa tumebaki na Sofa moja tu ambapo Brac wamesema watakuja kumalizia na Masufuria. Kazi yangu ni kubonda Kokoto ambayo Ndoo moja ni 1,000" - Mdaiwa, Mkoa wa Iringa.
"Kitendo hicho kilimuumiza sana kama Mama (tukiacha uanasiasa pembeni) nina hofu ya Mungu lakini pia kama mama nilijiuliza hawa watoto wangekuwa ni wa kwangu jinsi baba amewakumbatia katika shida, hakuamua kuwaacha" - Mhe. Oliver Semuguruka
"Nilimwambia yule Mzee nitamsaidia kulipa deni la kiasi kilichobaki. Nilimuambia Mwandishi wa Habari aende kwa yule mzee waende wanapodaiwa wapigiane mahesabu kisha aniletee Bili nimlipie"
"Niwasihi akina Mama, tuache tamaa ya kuchukua mikopo ambayo hatuwezi kuilipia" - Mhe. Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera
Yani nionee wivu upumbavu huu? Matumizi mabaya ya wivu yatakuwa sasa we fanya siaso majichoo kama hizi then njoo post tu kwa raha zako ila huna hatimiliki ya watu kufikiria wanavyotaka! Ungekuwa cha maana umefanya tangu umepewa na jiwe wala usingekuja kujitangaza hapa kwa kijimsaada ambacho watu tunafanya deile na inabaki moyoni kati yetu na Mungu. Anyway ni muda wa kurudisha hesabu so jiokotezee tu uwashawishi wakupe tena ukagonge meza huko!
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliver Semuguruka amefanya Kitendo cha Utu, huruma na mfano mzuri wa kuigwa baada ya kuamua kumlipia deni mkazi mmoja wa Mkoa wa Iringa aliyekumbiwa na mke wake kwasababu ya madeni ya Brac.
"Mke amekimbia ameniachia watoto, tulishauriana aende achukue mkopo ili tupate uwanja cha Tsh 300,000 au Tsh 400,000 ambapo marejesho ilikuwa kama Shilingi 15,000 kwa wiki lakini yeye alivyoenda alichukua 1,200,000 ambayo kwa wiki ni marejesho ya shilingi 38,000 ambayo nashindwa kuifikisha" - Mkazi wa Iringa (Mdaiwa)
"Walishachukua Sabufa, TV, na vitu vingine vimeisha. Mpaka sasa tumebaki na Sofa moja tu ambapo Brac wamesema watakuja kumalizia na Masufuria. Kazi yangu ni kubonda Kokoto ambayo Ndoo moja ni 1,000" - Mdaiwa, Mkoa wa Iringa.
"Kitendo hicho kilimuumiza sana kama Mama (tukiacha uanasiasa pembeni) nina hofu ya Mungu lakini pia kama mama nilijiuliza hawa watoto wangekuwa ni wa kwangu jinsi baba amewakumbatia katika shida, hakuamua kuwaacha" - Mhe. Oliver Semuguruka
"Nilimwambia yule Mzee nitamsaidia kulipa deni la kiasi kilichobaki. Nilimuambia Mwandishi wa Habari aende kwa yule mzee waende wanapodaiwa wapigiane mahesabu kisha aniletee Bili nimlipie"
"Niwasihi akina Mama, tuache tamaa ya kuchukua mikopo ambayo hatuwezi kuilipia" - Mhe. Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera View attachment 3153025
Hongera sana kwa Mheshimiwa Mbunge kumrudishia upya Furaha na Amani ya Moyo huyu Jamaa. Hakika nami natamani kukutana na huyu Jamaa kumtia Moyo zaidi. Namuona ni Mtu mwenye Maono makubwa na mafanikio siku za usoni. #BadoHatujaishiMpakaTukifanyaKituAmbachoTunayemfanyiaHaweziKutulipa